Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga: Waleteni hao KMC

45792 Pic+yangaa Yanga: Waleteni hao KMC

Mon, 11 Mar 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Kocha  wa Yanga,Mwinyi Zahera amesema kuelekea mechi yao ya kesho dhidi ya KMC wamewasoma wapinzani wao na sasa wako tayari kwa mchezo huo.

Zahera amesisitiza wamekamilisha maandalizi kuelekea mechi hiyo.

Mkongo huyo amesema wamejiandaa vyema kwa kuangalia wapi walikosea katika mchezo na wapi walipatia katika mechi iliyotangulia baina ya timu hizo.

Zahera ameongeza amesema hategemi mabadiliko makubwa kuelekea mechi hiyo kutokana na ugumu wa wapinzani wao.

Amesema amewaandaa vyema vijana wake kuelekea mechi hiyo na kwamba kama watashika walichowafundisha Yanga itapata matokeo mazuri.

Aliongeza katika kuelekea mechi hiyo kikosi chake kitamkosa mtu mmoja pekee kipa wake kinda Ramadhan Kabwili ambaye ameugua ghafla jana.



Chanzo: mwananchi.co.tz