Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga, UD Songo, KCCA zatangulia Shirikisho Afrika

77752 Pic+yanga

Sun, 29 Sep 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam.Yanga imeungana na timu nyingine sita zilizoondolewa katika Ligi ya Mabingwa na kuangukia hatua ya mtoano ya Kombe la Shirikisho Afrika baada ya jana, Jumamosi kufungwa na Zesco United kwa mabao 2-1.

Awali Yanga walishindwa kutumia faida ya kucheza nyumbani kwa kulazimishwa sare ya bao 1-1 na Zesco United ambayo inafundishwa na kocha wa zamani wa timu hiyo, George Lwandamina.

Yanga imeondolewa kwenye Ligi hiyo ya Mabingwa Afrika kwa jumla ya mabao 3-2  hivyo watapigania nafasi ya kuingia makundi ya kombe la shirikisho Afrika, wakiwa na wenzao, KCCA (Uganda), UD Songo (Msumbiji), Elect-Sport (Chad), Cano Sport (Equatorial Guinea), Al-Nasr (Libya), Côte d'Or (Shelisheli).

Yanga bado wana dakika nyingine 180 katika anga la kimataifa, kwani sasa imetupwa Kombe la Shirikisho na sasa wanasubiri kuja watacheza na nani.

Bao la kujifunga na kiungo fundi wa mpira, AbdulAziz Makame katika dakika ya 79, lilizima ndoto za Yanga kucheza makundi ya michuano hiyo kwa mara ya pili tangu walipofanya hivyo mwaka 1998.

Makame alijifunga wakati akiondoka krosi ya Mwila Phiri na kuifanya Yanga iondolewa kwa jumla ya mabao 3-2 na kumfanya kiungo huyo kumwaga chozi kama mtoto mara baada ya kumalizika kwa dakika 90 na kutulizwa na nyota wenzake na wale wa Zesco.

Pia Soma

Advertisement
Katika mchezo huo wa jana uliopigwa kwenye Uwanja wa Levy Mwanawasa mjini Ndola, Zambia Yanga iliyolazimishwa sare ya 1-1 nyumbani, iolicheza vyema, lakini ikauhusu bao dakika ya 25 na Jesse Were aliyefunga kwa kichwa akimzidi ujanja beki Lamine Moro aliyembana wakati akimalizia pasi ya kichwa ya Winston Kalengo.

Bao hilo lilidumu kwa dakika sita tu, kwani Yanga walisawazisha dakika ya 31 kupitia mshambuliaji Urikhob akimalizia mpira uliotemwa na kipa Jacob Banda wakati akitaka kuokoa krosi ya Makame shambulizi lililotokana na kona iliyopigwa na Patrick Sibomana.

Kipindi cha kwanza kilimalizika huku umiliki wa mpira ukiwa 50 kwa 50  na kipindi cha pili Zesco walirudi kwa kasi na dakika 52 beki Kelvin Yondani alifanya kazi ya ziada akiokoa mpira uliokuwa unaelekea ndani ya wavu uliotanguliwa kupanguliwa na kipa wake Metacha Mnata wakati akiokoa shuti la Kalengo aliyepewa pasi safi na Werre.

Wenyeji walilazimika kumtoa Ching’andu akiingia kiungo mkongwe Kondwani Mtonga badiliko ambalo liliwaimarisha hasa katika eneo la kiungo.

Ndipo katika dakika ya 79 Yanga walijikuta wanaruhusu bao la kujifunga kwa mguu wa kulia na Makame wakati akijaribu kuokoa krosi kali ya Phiri ikimtafuta Werre na kuifanya timu yake kuwa nyuma.

Kuingia kwa bao hilo kuliwalazimu Yanga kuwatoa Feisal Salum akiingia Juma Balinya, pia kumtia Ali Ali na kumuingiza Maybin Kalengo pia baadae akitoka Sibomana na kumpisha Mrisho Ngassa mabadiliko ambayo yalilenga kuongeza kasi ya masgambulizi kwa Yanga.

Dakika ya 90 Kalengo alipoteza nafasi akiwa na kipa baada ya kipa kupangua kisha mwamuzi Andofetra Rakotojana kudai mshambuliaji huyo alimchezea vibaya kipa huyo.

Vigogo hao saba wakiwa na Yanga, wanasubiri wenzao ambao wataondolewa leo kwenye michezo mingine ya marudiano ya Ligi ya Mabingwa Afrika ili kucheza hatua hiyo ya mchujo kuingia makundi ya shirikisho.

Michezo ambayo inatarajiwa kuchezwa leo kwenye Ligi ya Mabingwa ni kati ya Horoya ya Guinea ambayo itacheza na JS Kabylie ya Algeria, AS Vita Club dhidi ya ASC Kara, Al-Hilal ya Sudan itakuwa nyumbani kuikaribisha, Enyimba ya Nigeria.

Gor Mahia, ambayo inawachezaji wa Kitanzania, David Kissu na Dickson Ambundo wanamtiani wa kupindua matokeo ya mabao 4-1 mbele ya USM Alger huku Zamalek wakiwasubiri, Génération Foot ya Senegal.

Michezo mwingine utachezwa Tunisia kati ya Étoile du Sahel dhidi ya Asante Kotoko ya Ghana, Wydad Casablanca wanamtiani wakiwa kwao wa kukomboa mabao 2-0 mbele ya FC Nouadhibou ya Mauritania.

1º de Agosto ya Angola wanadaiwa bao moja leo wakiwa nyumbani ili kuwaondoa Green Eagles ya Zambia kutokana na mchezo wa kwanza ugenini kupoteza kwa mabao 2-1.

TP Mazembe wanayoichezea Watanzania, Ramadhan Singano na Eliud Ambokile wataikaribisha, Fosa Juniors ya Madagascar ambao walitoka nao suluhu kwenye mchezo wa kwanza.

Chanzo: mwananchi.co.tz