Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga, Simba zaweka nuksi kikosi cha Prisons

56301 Pic+prison

Wed, 8 May 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Michezo miwili ya Prisons ya hivi karibuni imekuwa shubiri kutokana na kupoteza mbele ya Yanga ilipokuwa Uwanja wa Uhuru na ule wa Sokoine jijini Mbeya mbele ya Simba.

Ni kama mzimu wa timu hizo mbili bado imeendelea kutalii ndani ya kikosi hicho cha wana jelajela jambo ambalo limevunja ukimya wa kocha wao huku akisema ishu sio wachezaji kucheza vibaya bali ni uchovu wa safari.

KOCHA Msaidizi wac Tanzania Prisons Ramadhani Katumba amaesema kilicho changia timu yake kupoteza mchezo kwenye uwanja wake wa nyumbani dhidi ya Simba imetokana na wachezaji kuwa na uchovu wa mchezo uliyopita dhidi ya Yanga uliyochezwa jijini Dar essalam siku ya Ijumaa.

Alisematimu yake ilimiliki mpira kwa nafasi kubwa ila walishindwa kutumia nafasi ambazo walikuwa wanapata kutokana kukosa utulivu wanapo karibia langoni.

“Tumetoka kucheza na Yanga Dar es Saalam na wakati tunarudi tulipata ajali na wachezaji wakawa na uchovu hivyo kukabili hali ya hewa ya mbeya ikatusumbua wakati huo wenzetu walishafika siku nyingi, hivyo ni baadhi ya vitu vilivyochangia na unajua mtu ukitoka safarini ukapata ajari mawazo yanakuwa ni mengi ila namshukuru Mungu mpira umechezwa vizuri samba wamepata bahati baada ya makosa ya beki wetu kutegeana na kipa na kupelekea wapinzani wetu kushinda, alisema Katumba.

 

 



Chanzo: mwananchi.co.tz