Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga, Simba, Azam zapishana ‘airport’

6f415487e92c03a9b5e547e5c0c9f4cd Yanga, Simba, Azam zapishana ‘airport’

Thu, 24 Jun 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

TIMU za soka za Yanga, Simba na Azam zimepishana kwenye Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA) zikienda katika mechi zao za nusu fainali ya Kombe la Shirikisho zitakazochezwa mwishoni mwa wiki.

Kikosi cha Yanga kilikuwa cha kwanza kufika kiwanjani hapo mapema alfajiri na kupanda ndege kwenda Tabora kwa ajli ya mchezo wao wa nusu fainali ya kombe hilo dhidi ya Biashara United ya Musoma mkoani Mara utakaofanyika kesho Ijumaa kwenye Uwanja Ali Hassan Mwinyi.

Akizungumza na HabariLEO, Meneja wa kikosi hicho, Hafidh Salehe amesema maandalizi yote yamekamilika na tayari walikuwa wameshatua mjini Tabora kwa ajili ya mchezo huo ambao wanatarajia kushinda.

Simba nao majira ya saa 2:00 asubuhi walipanda ndege kwenda Songea kwa ajili ya mchezo wao wa Jumamosi wa nusu fainali ya Kombe la Shirikisho dhidi ya Azam FC kwenye uwanja wa Majimaji mjini Songea.

Timu hizo kila moja imetamba kushinda mchezo huo na kutinga fainali itakayochezwa katika Uwanja wa Lake Tanganyika, Kigoma mwezi ujao.

Simba ndio bingwa mtetezi wa taji hilo na bingwa ndiye ataliwakilisha taifa katika michuano ya Kombe la Washindi barani Afrika msimu ujao utakaoanza Septemba, mwakani.

Katika michuano hiyo ya Kombe la Shirikisho Tanzania, Yanga iliwahi kuchukua mara moja msimu wa 2015/2016, Simba mara mbili 2016/2017 na 2019/2020, Mtibwa na Azam FC kila mmoja ilichukuwa mara moja 2017/2018 na 2018/2019.

Azam nao walifika kiwanjani hapo majira ya asubuhi n kukwea pia kuelekwa Songea kwa ajili ya mchezo huo na Simba.

Chanzo: www.habarileo.co.tz