Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga SC yawapa ambush wanajeshi Zanzibar

1112 Capture 10 TZW

Fri, 5 Jan 2018 Chanzo: bongo5.com

Klabu ya soka ya Yanga kutoka Tanzania bara imeiadhibu klabu inayomilikiwa na Jeshi la Kujenga Uchumi ya JKU kwa goli 1-0 kwenye michuano ya kombe la Mapinduzi inayoendelea visiwani Zanzibar.

Goli hilo la Yanga lililofungwa na Hassan Kessy kunako dakika ya 90 ya mchezo huo limeifanya klabu ya Yanga kufikisha pointi 6 kwenye kundi B.

Matokeo mengine ya mechi zilizochezwa mapema leo ni marudio ya mchezo wa Singida United dhidi ya Taifa Jang’ombe ulioahirishwa jana baada ya mvua kali kunyesha, ambapo Singida United wameibuka kidedea kwa ushindi wa goli 3-1.

Chanzo: bongo5.com