Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga SC yauteka mji, Majaliwa, Kikwete ndani

62799 YANGA+PIC

Sat, 15 Jun 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Habari ya mjini leo ni Yanga tu wakati Waziri Mkuu wa Jam-huri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa pamoja na Rais Mstaafu, Jakaya Kikwete watakapoongoza hafla maalum itakayorushwa mubashara na kituo cha televisheni cha Azam TV ya kuichangia klabu ya Yanga inayokwenda kwa jila la ‘Kubwa Kuliko’.

Wawili hao wataongoza kundi kubwa la vigogo wa serikali na taasisi binafsi, watu mashuhuri wakiwamo wasanii na na mamia ya wanachama wa klabu hiyo katika tukio hilo la kihistoria kuwahi kufanywa na klabu hiyo yenye mafanikio makubwa zaidi katika mchezo wa soka hapa nchini ikiwa imetwaa taji la Ligi Kuu Tanzania Bara mara 27.

Hafla hiyo ambayo ni mwendelezo wa kampeni ya kuichangia klabu hiyo ili ipate fedha za kuendesha usajili na kambi ya maandalizi kwa ajili ya msimu ujao, itafanyika kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee kuanzia saa 2.00 asubuhi hadi saa 11.00 jioni.

Taarifa iliyotolewa na Yanga jana ime-thibitisha kuwa Majaliwa na Rais Msta-afu Kikwete watahudhudhuria hafla hiyo ambayo itaendana na harambee ya kusa-ka kiasi cha Sh 1.5 bilioni.

“Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Kassim Majaliwa atakuwa Mgeni Rasmi katika Kubwa Kuliko na Mgeni Maalum atakuwa Rais Mstaafu Mheshimiwa Jakaya M. Kikwete,” ilisema taarifa hiyo.

Mbali ya Majaliwa na Kikwete, vigogo wengine ambao wanatarajiwa kushiriki hafla hiyo ni Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama, Jenerali Venance Mabeyo, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Utumishi na Utawala Bora), George Mkuchika, Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Miche-zo, Dk. Harrison Mwakyembe pamoja na Naibu Waziri, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu, Anthony Mavunde Ukiondoa hao wanatarajiwa kuwapo pia baadhi ya wakuu wa wilaya na mikoa wakiongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, Jokate Mwegelo na wabunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambao ni wapenzi na wanachama wa Yanga wakiongozwa na mbunge wa Kilolo (CCM), Venance Mwamoto.Kwa mujibu wa ratiba iliyotolewa na klabu hiyo, wageni waalikwa wataanza kuwasili kuanzia saa 2 asubuhi na mgeni rasmi atawasili mnamo saa 4.40 asubuhi.

Pia Soma

Kisha kufuatiwa na matukio mengine kul-ingana na ratiba hiyo ilivyopangwa.Mapema juzi, mwenyekiti wa Kamati Ndogo ya Uhamasishaji ya Yanga, Dk. David Ruhago alisema kadi za kushiriki tukio hilo zinapatikana katika maeneo mbalimbali na kwenye mitandao kwa bei ya Sh.50,000, 100,000, mil. 5 na mil. 10/-.

Chanzo: mwananchi.co.tz