Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga SC yalia na ratiba ya ligi kuu VPL

3802 Ten 1 1 TZW

Tue, 27 Feb 2018 Chanzo: bongo5.com

Kikosi cha mabingwa watetezi wa ligi kuu soka Tanzania Bara Dar es salaam Young African kinatarajia kusafiri asubuhi ya leo kuelelea Songea tayari kwa mchezo wa kombe la ASFC dhidi ya wenyeji Majimaji Fc.



Kuelekea katika mchezo huo Ofisa habari wa klabu hiyo, Dismas Ten amesema kuwa,Yanga inasafiri kuelekea Songea kwa ndege lakini kukiwa na shaka kubwa kikosini juu ya ‘mmbanano’ wa ratiba kwa michezo inayofuata ya kikosi chake .

Tutacheza Songea tarehe 25 kisha Mtwara tarehe 28 halafu Morogoro tarehe 3 hii si ratiba rafiki hasa ukizingatia tuna mchezo wa ligi ya Mabingwa tarehe 6.

Tunajaribu kuwasiliana na Shirikisho la soka kuomba kusogezwa mbele kwa mchezo wa Morogoro ili tupate muda wa kujiandaa kabla ya kucheza na Township Rollers ya Botswana.

Chanzo: bongo5.com