Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga SC wafikia hatua nzuri Jangwani (+Video)

653 Capture 71 TZW

Wed, 27 Dec 2017 Chanzo: bongo5.com

Klabu ya Yanga imeanza matengenezo ya uwanja wake wa Kaunda uliopo makao makuu ya klabu hiyo eneo la Jangwani Jijini Dar es Salaam.

Kupitia ukurasa wao wa  Instagram Mabigwa hao watetezi wameweka video ikionesha ukarabati ukiendelea katika uwanja huo na kuandika”Nusu ya uwanja iko karibu kufikiwa“.

Uwanja wa Kaunda au kama wengi walivyozoea kuuita Jagwani ulijengwa mwaka 1973 kwa gharama ya tsh milioni 3 ambazo zilipatikana kwa michango kutoka kwa taasisi mbalimbali na wahisani wengine.

Mapema mwaka huu klabu ya Yanga iliwaomba pia wadau na mashabiki wake waichangie klabu hiyo ili kuukarabati uwanja huo wa kaunda pamoja na kujenga hosteli za kisasa za wachezaji. Tazama Video hiyo inayoonesha Greda likisawazisha vifusi vilivyokuwa vimemwagwa uwajani hapo kwa siku kadhaa zilizopita

Nusu ya uwanja iko karibu kufikiwa..! #asantekwasupport #asantekwakuchaguakuwabingwa #tukutaneccmkirumba @mbaofc vs @yangasc #31desemba #kalendar2018 #zitakuwepo #patanakalayakosasa #merrychristmas #happynewyear

A post shared by Young Africans SC (@yangasc) on Dec 25, 2017 at 5:22am PST

Chanzo: bongo5.com