Klabu za soka kutoka Tanzania Bara, Yanga SC na Simba SC jana zilitupa karata zao za kwanza kwenye michuano ya Kombe la Mapinduzi visiwani Zanzibar kwa kupata matokeo.
Juma Mahadhi
Mchezo wa kwanza ulianza kati ya Simba SC na Mwenge SC ambapo hadi dakika za mwisho mchezo ulimalizika kwa matokeo ya sare ya goli 1-1 .
Goli la Simba SC limefungwa na Jamali Mwambeleko kunako dakika ya 2 ya mchezo kabla ya Humoud kusawazisha goli hilo dakika ya 28.
Mchezo mwingine uliopigwa jana usiku ni kati ya Yanga SC na Mlandege ya Zanzibar ambapo matokeo yalikuwa ni ya ushindi kwa Yanga wa goli 2-1 .
Magoli ya Yanga SC yote yalifungwa na Juma Mahadhi na goli pekee la kufutia machozi la Mlandege lilifungwa na Omary Makame.
Tazama ratiba ya leo Januari 03, 2017 ya michuano ya Kombe la Mapinduzi ;