Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga SC bado wakomalia ishu ya Morrison

E3BE5419 BC1B 4E46 93DF D759DC681EC8 660x400.jpeg Yanga SC bado wakomalia ishu ya Morrison

Thu, 1 Oct 2020 Chanzo: millardayo.com

Club ya Yanga SC kupitia makamu mwenyekiti wao Fredrick Mwakalebela leo amesema kuwa mchezaji Bernard Morrison kwenye mfumo wa FIFA wa usajili Morrison bado anasomeka kuwa ni mchezaji wao Yanga.

Mwakalebela anasema mkataba wa Simba na Morrison una mapungufu sababu hauna saini ya kiongozi wa Simba zaidi ya Morrison mwenyewe hivyo Morrison bado ni mchezaji wao.

“Kwa maana hiyo mkataba wa Morrison ukiangalia kwa karibu kwa jicho la kisheria na mtu wa kawaida unaonekana kuwa umesainiwa na upande mmoja, kwa maana hiyo inaonesha kuwa Simba SC ya Dar es Salaam haijaridhia mkataba wa Morrison kwa sababu hakuna sehemu yoyote ambapo club ya Simba imesaini mkataba”>>> Mwakalebela

Kama utakuwa unakumbuka vizuri kamati ya sheria na hadhi za Wachezaji ya TFF baada ya Morrison kukana kuwa na mkataba na Yanga, walipitia na kujiridhisha kuwa mchezaji huyo ni huru ikiwa ni siku chache zimepita akiwa ametoka kutangazwa kusaini Simba SC.

Chanzo: millardayo.com