Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga, Mwadui mechi ya presha

Acc222a1e99285b4e1b97e2e0936b15b Yanga, Mwadui mechi ya presha

Sat, 18 Jul 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

MABINGWA wa kihistoria Yanga leo wana kazi nyingine ngumu ya kuwakabili Mwadui katika mchezo utakaochezwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Mchezo huo unaweza kuwa wenye presha kwasababu kila mmoja anahitaji matokeo, Yanga inataka kubaki katika nafasi ya pili ambapo kwa sasa ina pointi 67 na Mwadui wanataka kujiondoa kwenye mstari wa kushuka daraja wakishika nafasi ya 17 kwa pointi 40. Timu hizo mara ya mwisho zilikutana kwenye mzunguko wa kwanza na Yanga ikiwa ugenini

Shinyanga ilishinda bao 1-0.

Huenda morali ya Yanga ikaendelea kuwa bora baada ya mchezo uliopita kushinda mabao 3-1 dhidi ya Singida United. Ila kwa Mwadui wanaweza kuwa na hasira ya kutaka matokeo mazuri kutokana na kupoteza mchezo uliopita dhidi ya Ruvu Shooting mabao 3-2. Kocha wa  Yanga, Luc Eymael amekuwa akijaribu kubadilisha wachezaji kwenye kikosi cha kwanza kwa kuwapumzisha baadhi na kuwaweka ambao walikuwa hawapati nafasi ya  kucheza na hilo alilionesha katika mchezo uliopita.

Licha ya kujitahidi kufanya vizuri mabingwa hao wa kihistoria bado wanaonekana wana tatizo katika safu ya ushambuliaji ambako inatengeneza nafasi nyingi na kufunga mabao machache na hilo Eymael amekuwa akilizungumzia. Pia, katika safu ya ulinzi wamekuwa wakiruhusu mabao kuonesha wazi hakuna maelewano mazuri kati ya mabeki na kipa.

Mbali na mchezo huo, Namungo inatarajiwa kucheza na maafande wa Tanzania Prisons kwenye Uwanja wa Majaliwa. Timu hiyo ya Ruangwa imekuwa katika mwenendo mzuri na mara ya mwisho kukutana Sokoine Mbeya ilishinda mabao 3-2.

Namungo inayoshika nafasi ya nne kwa pointi 63 ni moja ya timu zinazovizia nafasi ya pili na ikiwa wataendelea kushinda na walioko juu yake Azam na Yanga wakateleza, basi yeye inaweza kupanda na kufanya mapinduzi. Lakini pia, Prisons inayoshika nafasi ya 11 kwa pointi 44 kama itaruhusu kupoteza mchezo huo itakuwa kwenye hatari ya kushuka chini.

Mechi nyingine ngumu ni Ndanda dhidi ya Mbeya City, utakaochezwa kwenye Uwanja wa Nangwanda Sijaona Mtwara. Timu zote mbili ziko kwenye mstari wa kushuka daraja. Ndanda inashika nafasi ya 15 kwa pointi 40 na Mbeya City 18 kwa pointi 39 hivyo, kila mmoja anahitaji matokeo mazuri kujion

doa waliko.

Mtibwa inayoshika nafasi ya 13 kwa pointi 41 itachuana na KMC  inayoshika nafasi ya 12 kwa pointi 43 kwenye Uwanja wa CCM Ahmed Gairo na zote zikiwa hazina uhakika wa kubaki salama, kwani ziko karibu na mstari wa kushuka. Kila mmoja anahitaji matokeo mazuri.

Timu nyingine ambazo pia zinahitaji kupambana ni Kagera Sugar itakayocheza  dhidi ya  Polisi Tanzania kwenye Uwanja wa Kaitaba, Biashara United dhidi ya Coastal Union kwenye Uwanja wa Karume, Mara na Ruvu Shooting dhidi ya Singida United Mabatini, Mlandizi.

 

Chanzo: habarileo.co.tz