Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga, Mwadui  kusuka au kunyoa 

97c7fe51a76c32d52c9224f9fdd6b272.png Yanga, Mwadui  kusuka au kunyoa 

Tue, 25 May 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

MCHEZO wa pili wa robo fainali ya Kombe la Shirikisho la Azam utapigwa leo mkoani Shinyanga kati ya Mwadui FC na Yanga katika uwanja wa CCM Kambarage.

Yeyote kati ya timu hizo atayepoteza mchezo huo atakuwa ameyaaga mashindano hayo hali inayoongeza ugumu wa mtanange huo.

Biashara United imekuwa timu ya kwanza kutinga hatua ya nusu fainali ya michuano hiyo baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Namungo FC, mchezo uliopigwa juzi katika Uwanja wa Karume mjini Musoma.

Yanga leo itashuka uwanjani kuwakabili Mwadui FC ikiwa na kumbukumbu nzuri ya kuondoka na ushindi mnono wa mabao 5-0 katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara mzunguko wa kwanza.

Yanga imetinga hatua ya robo fainali ya Kombe la Shirikisho la Azam baada ya kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Tanzania Prisons, wakati Mwadui FC iliwafunga Coastal Union kwa mabao 2-0.

Akizungumza na gazeti hili, Kocha Nasreden Nabi alisema maandalizi ya kikosi chake kwa ajili ya mchezo huo yamekamilika kipo vizuri japokuwa hawezi kuwadharau wapinzani wao kwani hatua ya mtoano mara nyingi imekuwa ikitoa matokeo ya kushangaza.

Alisema kutokana na jinsi walivyojipanga ana amini wanaenda kushinda mchezo huo na kutinga nusu fainali.

“Malengo yetu msimu huu ni ubingwa wa Ligi Kuu pamoja na Kombe la Shirikisho la Azam, hivyo tutaingia uwanjani tukiwa na lengo moja tu la kusaka ushindi ili kujiweka katika mazingira mazuri ya kulikaribia taji.”

“Tumekuwa na matokeo mazuri dhidi yao, tumeshinda mchezo uliopita hali ya kikosi iko sawa wachezaji wanaendelea vizuri, naamini tunaenda kushinda na kuingia hatua ya nusu fainali,” alitamba Nabi

Naye Kocha Mkuu wa Mwadui FC, Salhina Mjengwa alisema anaiheshimu Yanga ni timu kubwa yenye mashabiki wengi na anajua kuwa utakuwa mchezo mgumu kutokana na kila timu kuhitaji kuingia nusu fainali, lakini hawako tayari kupoteza michezo miwili kwa timu moja katika uwanja wa nyumbani.

“Wachezaji wangu wana morali ya hali ya juu, tutaingia katika mchezo huu tukiwa na matumaini makubwa ya kuibuka na ushindi na kuingia hatua ya nusu fainali kwani ndio tumaini lililobaki kwetu.”

“Tulipoteza mchezo wa kwanza nyumbani dhidi yao hivyo hatutakubali kupoteza mara mbili dhidi yao,” alisema Mjengwa.

Mwadui tayari imeshuka daraja kutoka Ligi Kuu Tanzania Bara baada ya kujikusanyia pointi 19 tu katika michezo 30 na hata kama itashinda mechi zote sita zilizobaki haiwezi kupona.

Chanzo: www.habarileo.co.tz