- ya pande mbili hizo, imeelezwa.
Awali ilielezwa Lamine amesimamishwa kwa muda usiojulikana na Nabi baada ya kuwapo kwa vitendo vya utovu wa nidhamu, jambo ambalo beki huyo alilikataa na kuutaka uongozi uweke taarifa sahihi juu yake.
Akizungumza na gazeti hili jijini Dar es Salaam jana, Kaimu Katibu Mkuu wa Yanga, Haji Mfikirwa alisema baada ya nyota huyo kusimamishwa, viongozi walikutana na Nabi pamoja na mchezaji huyo kwa lengo la kusikiliza hoja za kila upande na hatimaye kuweka mambo sawa.
Mfikirwa alisema uongozi ulilazimika kulifanyia kazi suala hilo kwa sababu linahitaji kuona kila mchezaji anafuata taratibu na kanuni za klabu hiyo kikamilifu.
“Tulisikiliza hoja za pande zote mbili, tulikutana na Lamine wakati timu mkoani, baadaye tukazungumza na kocha (Nabi), hivyo tumefanyia kazi hoja zao na sasa mambo safi na Lamine yuko kambini Avic Town, Kigamboni, akiendelea na mazoezi kwa ajili ya michezo yetu ijayo,” alisema Mfikirwa.
Kutokana na adhabu aliyokuwa anaitumikia, Lamine alikosa mechi mbili za Ligi Kuu Bara dhidi ya Namungo FC na JKT Tanzania pamoja na mchezo wa hatua ya robo fainali mashindano ya Kombe la FA dhidi ya Mwadui.