Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga, Azam FC zauota ubingwa

YANGA.png?fit=743%2C385&ssl=1 Yanga, Azam FC zauota ubingwa

Tue, 27 Apr 2021 Chanzo: ippmedia.com

Wakati Niyonzima akisema hayo, Ofisa Mtendaji Mkuu wa Azam,  Abdulkarim Amin 'Popat' na nahodha wake, Aggrey Morris wamesema wataendelea kupambana kwa mechi zilizosalia ili kujiweka katika nafasi nzuri ya kutwaa ubingwa kwa sababu bado mbio za kuwania taji hilo ziko wazi.

Niyonzima aliliambia gazeti hili kikosi chao kilicheza vizuri lakini kosa moja walilofanya liliwaruhusu Azam kulitumia vyema na kujipatia bao hilo la ushindi.

"Ni mbaya sana kukata tamaa. Tumecheza vizuri, tumeadhibiwa kutokana na kosa tulilofanya. Bado naamini tunaweza kuchukua ubingwa. Tuna mechi mkononi na hawa Azam pamoja na Simba wanaweza kupoteza vile vile," alisema Niyonzima.

Kiungo na nahodha huyo wa Timu ya Taifa ya Rwanda, aliwataka wachezaji wenzake kuendelea kushikamana katika kipindi hiki na wafahamu ni dhambi kukata tamaa.

"Kama hujafika mwisho wa kile unachopaswa kukifanya, hupaswi kukata tamaa," alisema Niyonzima.

Popat alisema matokeo ya mechi ya mzunguko wa kwanza ambayo timu yake ilifungwa bao 1-0 yalimuumiza sana, lakini sasa maumivu yake yamekwisha.

"Wao walichukua tatu kwetu na sisi tumechukua kwao. Azam tulianza vizuri, tukatetereka na sasa tunamaliza vizuri. Tutapambana hadi dakika za mwisho kwa sababu bingwa bado hajatangazwa. Mwisho wa ligi ndiyo tutajua, lakini kwa sasa bado tunasaka ubingwa," alisema Popat.

Aggrey Morris, nahodha wa Azam FC alisema timu zote mbili zilicheza vizuri na mashabiki walifurahia kandanda safi huku akiongeza ligi bado haijamalizika na chochote kinaweza kutokea katika michezo iliyobakia ya lala salama.

Chanzo: ippmedia.com