Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga, Alliance kitawaka

49548 PIC+YANGA

Mon, 1 Apr 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Mwanza. Usiulize Alliance FC itakuwa na kibarua kizito cha kulipiza kisasi pale watakapowavaa Yanga katika mchezo wa Robo Fainali ya Kombe la FA kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini hapa.

Katika mchezo uliopita wa Ligi Kuu uliopigwa kwenye uwanja huo hivi karibuni Alliance ilikubali kichapo cha bao 1-0 kutoka kwa Yanga.

Mchezo huo unatarajiwa kuwa mkali zaidi kwani Alliance hawatakubali kuchezea kichapo tena hicho huku Yanga wakitaka kutinga nusu fainali ya kombe hilo.

Tayari Yanga wako jijini hapa tangu juzi Alhamisi na jana jioni walitarajiwa kufanya mazoezi ya mwisho katika uwanja wa CCM Kirumba tayari kwa mchezo huo.

Alliance wajiapiza kulipiza kisasi

Kocha Msaidizi wa timu hiyo, Kessy Mzirai, alisema kikosi chao kipo fiti kuwavaa Yanga katika mchezo huo ambao alisema hawatokubali kupoteza.

Alisema sasa wamewajua vizuri Yanga na wanajua udhaifu wao hivyo hawana presha kuelekea katika mchezo huo wa leo.

“Tunajua mchezo utakuwa mgumu, lakini tunataka kulipiza kisasi na pia msimu huu tumejipanga kuhakikisha tunafika fainali ya Kombe la FA na hatimaye kunyakua ubingwa,” alisema Mzirai.

Alisema wachezaji wa kikosi hicho wana morali ya juu kuelekea mchezo huo na wamedhamiria kuweka rekodi kwa kuwafunga Yanga kwa mara ya kwanza.

Bigirimana mzuka mwingi

Straika wa Alliance, Bigirimana Blaise, alisema wachezaji wako fiti kuelekea mchezo huo ambao anaamini licha ya kuwa mgumu watapata ushindi.

Alisema walikuwa wanatamani sana kupangwa dhidi ya Yanga jambo ambalo limetoea hivyo na sasa wanataka kuonyesha kuwa wako vizuri kwa kushinda mchezo huo.

“Ni mchezo mgumu sana kuliko uliopita hapa atakayefungwa atakuwa ameyaaga mashindano, hivyo tumejipanga na tuko fiti kwa ajili ya mpambano huu,” alisema Blaise.

Zahera afunguka

Kocha Mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera, amesema mchezo wa leo dhidi ya Alliance ni muhimu na wamejipanga kushinda.

Alisema wanawafahamu uwezo wa wapinzani wao lakini hana hofu na nyota wake. “Utakuwa ni mchezo mzuri kwa timu zote, tumekuja kutafuta nafasi ya kusonga mbele na natumai tutaingia nusu fainali,” alisema Zahera.

Kamusoko na Mohamed wapania mchezo

Kiungo wa Yanga, Thaban Kamusoko, alisema kuwa mchezo wao wa leo utakuwa mgumu lakini kutoka na moraki waliyonayo pamoja na dhamira yao kwenye michuano hiyo lazima washinde.

Alisema kuwa pamoja na kuwakosa baadhi ya nyota wenzao ambao kimsingi wangesaidia chochote, lakini hata waliopata bahati ya kuungana na timu watafanya vizuri. “Tunawakabili Alliance kwa tahadhari lakini kwa kujiamini. Tuliwafunga katika mechi ya mwisho tuliyokutana nao, kwahiyo kikubwa ni kupambana kila mmoja wetu ili kutimiza malengo,” alisema Kamusoko. Kwa upande wake winga wa kushoto, Jafary Mohamed alisema kuwa kutokana na maandalizi waliyoyafanya lazima wafanye kweli na kwamba wanawaheshimu Alliance lakini hawawaogopi.

Yanga itawakosa Ibrahim Ajibu ambaye hakufanya mazoezi na timu kwa madai ya afya yake kutokuwa sawa.

Wengine ni beki wa kushoto, Gadiel Michael ambaye ameenda Afrika Kusini kwa majaribio ya kucheza soka la kulipwa, na lipa Ramadhan Kabwili ambaye yuko na timu ya Taifa ya Vijana U-20 ‘Ngorongoro Heroes’ na beki wa kati Abdalah Shahibu ‘Ninja’ ambaye anatumikia adhabu ya kufungiwa.

Alliance wao watawakosa wachezaji watatu ambao ni Juma Nyangi aliyefungiwa mechi tatu, Israel Patrick na Hans Msonga ambao wameitwa  timu ya Taifa ‘Ngorongoro Heroes’.



Chanzo: mwananchi.co.tz