Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yacouba aipeleka Yanga fainali, baada ya miaka 5

Yacuba Yacouba aipeleka Yanga fainali, baada ya miaka 5

Sat, 26 Jun 2021 Chanzo: eatv.tv

Klabu ya Yanga ya Dar es salaam imetinga hatua ya fainali ya michuano ya kombe la Azam Sports Federation Cup baada ya miaka mitano, kufuatia ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Biashara United Mara kwenye mchezo wa nusu fainali uliochezwa uwanja wa Ali Hassan Mwinyi mkoani Tabora.

Bao pekee la Yanga kwenye mchezo huo limefungwa na Yacouba Sogne dakika ya 22 ya mchezo baada ya kupokea pasi ya upendo kutoka kwa kiungo mshambuliaji Feisal Salum ‘Fei Toto’. Mara ya mwisho Yanga kucheza fainali ya michuano hii ilikuwa msimu wa 2015-16 ambapo waliibuka mabingwa kwa kuifunga Azam FC, mabao 3-1.

Kwenye mchezo wa fainali timu ya Wananchi watacheza na mshindi wa mchezo wa nusu fainali ya Pili itakayo chezwa kesho Juni 25, 2021, huko Songea mkuani Ruvuma kwenye uwanja wa Majimaji ambapo Mabingwa watetezi Simba Sc watakuwa wakicheza na Azam FC.

Mchezo wa fainali ya michuano hii msimu huu utachezwa uwanja wa Lake Tanganyika mkoani Kigoma

Chanzo: eatv.tv