Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

YALIYOJIRI NOVEMBA 2018: Magori ateuliwa Mtendaji Mkuu Simba

34062 MAGORI+PIC Tanzania Web Photo

Mon, 31 Dec 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Novemba Mosi

Bangi yamponza kiungo Yanga

Kamati ya Kupambana na Kuzuia Dawa zisizoruhusiwa michezoni Kanda ya Tano(RADO) ilimfungia kiungo Mohammed Issa’Banka’ kutojihusisha na soka kwa miezi 14.

Banka alisajiliwa na Yanga akitokea Mtibwa Sugar na alifanyiwa vipimo akiwa Kenya alipokwenda kushiriki mashindano ya Chalenji akiwa na Zanzibar Heroes ndipo alipogundulika anatumia Bangi.

Novemba 4

Magori aula Simba

Crescentius Magori ameteuliwa kuwa Mtendaji Mkuu (CEO) wa klabu ya Simba wa Simba wakati Swedi Nkwabi akichaguliwa kuwa Rais wa klabu hiyo.

Viongozi hao walichaguliwa katika uchaguzi mkuu wa klabu hiyo uliofanyika kwenye Ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini.

Wanachama wa Simba waliweka historia katika uchaguzi huo baada ya kuingia katika mfumo mpya wa kuendesha klabu kutoka katika nguvu ya wanachama mpaka kwenye mfumo wa hisa ambao utaongoza na Mohammed Dewji’Mo’.

Novemba 6

Kuuli afungiwa maisha

Kamati ya Maadili ya Shirikisho la Soka Tanzania(TFF) ilimfungia maisha kutojihusisha na soka aliekuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ya Shirikisho hilo,Wakili Revocutus Kuuli.

Tangu alipotangaza kusimamisha mchakato wa uchaguzi wa klabu ya Simba kwa madai ya kutofuatwa kwa baadhi ya taratibu na kanuni za uchaguzi ndipo wakili huyo alipoanza kuingia matatani.

Novemba 13

Kigogo Yanga afungiwa

Mwenyekiti wa Matawi wa klabu ya Yanga Bakili Makele na Katibu wake Boaz Ikupilika walifungiwa miaka mitatu na Kamati ya Maadili ya TFF kutojihusisha na soka ndani na nje ya nchi.

Viongozi hao wa matawi walifungiwa kwa madai ya kuongea na vyombo vya habari na kupinga uchaguzi wa Yanga kusimamiwa na TFF huku wakifahamu yalikuwa ni maelekezo ya Baraza la Michezo Taifa(BMT) chombo kinachosimamia michezo nchini.

Novemba 21

Manji ndio basi tena Yanga

Licha ya kwamba aliandika barua ya kujiuzuru nafasi yake ya Uenyekiti wa Yanga tangu mwezi Juni mwaka jana na kisha kutengua umamuzi wake na kurejea katika nafasi yake lakini kutoonekana kwa jina lake katika majina ya wagombea katika uchaguzi ujao wa klabu hiyo kulihitimisha safari ya mfanyabiashara huyo ndani ya klabu hiyo.

Kutokana na kubanwa kila pande, wanachama na mashabiki wengi wa Yanga walifikiri Manji angechukua fomu ya kuwania tena nafasi yake katika uchaguzi utakaofanyika Januari 13 lakini hadi siku hii ya mwisho majina ya wagombea wakitangazwa jina lake halikuwepo.

Hata hivyo bado kuna mvutano wa chinichini kati ya Yanga na Shirikisho la Soka Tanzania(TFF) kuhusu uhalali wa nani anatakiwa kusimamia na kuendesha uchaguzi huo ingawa tayari Waziri wa Habari, Sanaa,Utamaduni na Michezo,Harrison Mwakyembe ameshatoa tamko kuwa uchaguzi wa klabu hiyo utafanyika kama ulivyopangwa na utasimamiwa na Kamati ya Uchaguzi ya TFF.

Novemba 28

Kibaya awalipa Samatta, Ngassa

Mshambuliaji wa Mtibwa Sugar, Jaffary Kibaya aliingia katika rekodi kwenye Kombe la Shirikisho Afrika baada ya kufunga mabao matatu hat-trick katika mchezo dhidi ya Northern Dynamo ya Shelisheli.

Mabao hayo yamemfanya aingie katika anga za Mbwana Samatta na Mrisho Ngassa.

Ngassa na Samatta ndiyo walikuwa Watanzania pekee kufunga mabao matatu na zaidi kwenye mchezo mmoja wa mashindanoya Afrika kwa ngazi ya klabu na hakuna mwingine aliyewahi kufanya hivyo.



Chanzo: mwananchi.co.tz