Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

YALIYOJIRI MEI 2018: JPM aikabidhi Simba taji, akiwapa makavu

Mon, 24 Dec 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Mei Mosi

Hanspoppe asakwa

Makahama ya Hakimu Mkazi Kisutu ilitoa amri ya kukamatwa kwa mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba, Zacharia Hanspoppe.

Hanspoppe alitakiwa kukamatwa ili kuunganishwa katika kesi ya utakatishaji fedha na kughushi inayowakabili waliokuwa viongozi wa Simba, Rais Evance Aveva na makamu wake, Geofrey Nyange ‘Kaburu’.

Mei 6

Failuna ashinda Tulia Marathon

Mwanariadha wa Tanzania Failuna Abdi alishinda mashindano ya Tulia Marathoni yaliyofanyika jijini Mbeya.

Failuna aliyemshinda Mkenya Christina Kambua alisema alipambana huku akikumbuka machungu ya kushindwa na wakenya kila mara kwenye mashindano mbalimbali aliyoshiriki.

Mei 8

Tambwe aanza kuozea benchi

Mshambuliaji Amiss Tambwe alikaa nje ya uwanja mwaka mzima akiuguza ugonjwa ambao mwenyewe alikuwa hauelewi.

Tambwe alisema alipitia kipindi kigumu katika maisha yake ya soka kwani madaktari walishindwa kubaini ugonjwa uliomsumbua hadi alipoamua kugeukia katika maombi ndipo alipopona.

Alisema alianza kupata maumivu ya goti la kushoto akiwa kambini Zanzibar walipokuwa wakijiandaa na mchezo wa Ngao ya Jamii dhidi ya Simba mwaka jana lakini licha ya kuhangaika hospitali nyingi kutafuta matibabu ikiwemo upasuaji madaktari hawakubaini tatizo.

Tambwe alisema wakati mwingine akiwa nyumbani alikuwa hapati maumivu lakini akirudi kambini tu kujiunga na wenzake mazoezini goti linaanza kuuma.

Mei 17

Mo akubaliana na Simba

Baada ya mvutano wa muda mrefu hatimaye bilionea Mohammed Dewji ‘Mo’ alikubali kufuata matakwa ya Serikali ya kuwekeza kwa asilimia 49 tu ndani ya klabu ya Simba ili asilimia 51 ziwe za wanachama wengine wa klabu hiyo.

Kulikuwa na mvutano, Mo akitaka apewe nafasi ya kumiliki hisa za klabu hiyo kwa asilimi 51 na 49 zibaki kwa wanachama wengine lakini Serikali akaingilia kati na kumpinga ikimtaka yeye amiliki asilimia 49 na zilizobaki ziwe za wanachama wengine, ingawa yeye bado atabaki kuwa na uamuzi wa mwisho.

Mei 19

Dk Magufuli aipa Simba madongo

Baada ya miaka mitano ya machungu hatimaye Simba ilitwaa ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara na kukabidhiwa taji lake na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, John Magufuli.

Ubingwa wa mwisho kwa Simba iliutwwa 2011/2012 na ubingwa ukabaki kutwaliwa an watani zao Yanga ikipokezana na Azam FC.

Simba ilitwaa ubingwa huo baada ya kumaliza Ligi ikiwa na pointi 69, kutokana na michezo 30 iliyocheza, ikishinda 20, sare tisa na kupoteza mmoja dhidi ya Kagera Sugar ilipochapwa bao 1-0 kwenye Uwanja wa Taifa mbele ya Rais Magufuli.

Kipigo hicho kikamfanya Rais Magufuli kuwatolea uvivu akiwaambia bado hawana kikosi cha kucheza mechi za kimataifa licha ya kutwaa ubingwa, akiwataka wajipange na wasiendelee kumuangusha yeye, mashabiki wao na Watanzania kwa ujumla.

Simba ndiyo mwakilishi wa Tanzania Ligi ya Mabingwa Afrika.

Mei 21

Kocha Tenisi aula Shelisheli

Kocha wa mchezo wan Tenisi hapa nchini, Nicolas Leringa alipata kazi ya kuifundisha timu ya Taifa ya Shelisheli.

Lelinga aliyekuwa kocha wa klabu ya Gymkhana Arusha aliingia mkataba wa miaka miwili na Chama cha Tenisi Shelisheli (STA)

Kocha huyo alisema Shelisheli walimuona baada ya kukunwa na uwezo wake alpotumia miaka 10 akifundisha tenisi nchini humo.

Mei22

Kiganja ahamishiwa kwa Waziri Mkuu

Aliyekuwa Katibu Mkuu wa Baraza la Michezo Tanzania (BMT) Mohammed Kiganja aliondolewa katika nafasi hiyo na kuhamishiwa Ofisi ya Waziri Mkuu.

Kiganja alihamia ofisi ya Waziri Mkuu akiwa Mkurugenzi wa Maadhimisho ya sherehe za kitaifa kutokana na utendaji mzuri akiwa BMT.

Mei 24

Wawili wafuzu Olimpiki

Waogeleaji Sonnia Tumiotto na Dennis Mhina walifuzu kuiwakilisha nchi kwenye mashindano ya Olimpiki ya vijana yaliyofanyika Argentina Oktoba mwaka huu.

Waogeleaji hao walifuzu baada ya kuweka rekodi ya muda katika mashindano ya Dunia yaliyofanyika nchini Hungary.

Mei 28

Njombe, Maji Majimaji zashuka

Timu za Njombe Mji na Majimaji ya Songea zilishuka hadi Ligi Daraja la Kwanza baada ya kufanya vibaya kwenye Ligi Kuu Tanzania Bara msimu uliopita.

Sare ya bao 1-1 dhidi ya Simba katika mchezo wa mwisho wa kufunga msimu ilihitimisha safari ya Majimaji kwenye Ligi Kuu Bara wakati Njombe Mji ilishushwa kwa kufungwa mabao 3-0 na Mwadui FC katika mchezo wa mwisho.



Chanzo: mwananchi.co.tz