Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

YALIYOJIRI JULAI 2018; Simba yaipiga Yanga bao, yamnasa Kagere

33522 Pic+kagere Tanzania Web Photo

Wed, 26 Dec 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Julai 5

CAF yaitoa Mtibwa Sugar kifungoni

Shirikisho la Soka Afrika (CAF) limeipa nafasi Mtibwa Sugar ya kushiriki mashindano ya kimataifa baada ya kuifungia miaka mitatu.

Mtibwa Sugar ilifungiwa miaka mitatu kutoshiriki mashindano yoyote yanayosimamiwa na CAF ngazi ya klabu baada ya mwaka 2002 kuingia mitini katika mchezo wa marudiano dhidi ya Santos ya Afrika Kusini.

Mchezo wa kwanza Mtibwa Sugar ilifungwa mabao 3-0 jijini Dar es Sakaam lakini haikwenda Afrika Kusini kwenye mchezo wa marudiano kwa madai haikuwa na fedha za usafiri.

Julai 7

Kim Poulsen awaacha TFF njia panda

Aliyekuwa mshauri wa ufundi wa timu za Taifa za soka za vijana, Kim Poulsen alijiuzuru nafasi hiyo kwa madai ya kupata changamoto mbalimbali licha ya kufanya kazi kubwa ya kuendeleza vipaji.

Alisema amevumilia mambo mengi hadi kufikia uamuzi huo na hakuona haja ya kubainisha kwa kila mtu nini kimempata zaidi ya kujiuluzu na kuwaacha waendelee na soka yao.

Julai 8

Miaka 55 Ubelgiji haijaifunga Brazil

Ushindi wa mabao 2-1 ilioupata Ubelgiji katika mechi ya robo fainali ya Kombe la Dunia dhidi ya Brazil ulikuwa wa kwanza baada ya miaka 55 kupita. Mara ya mwisho Ubelgiji kuifunga Brazil ilikuwa mwaka 1963 katika mchezo wa kirafiki uliofanyika mjini Brussels na wenyeji kushinda mabao 5-1.

Julai 16

Ufaransa mabingwa Kombe la Dunia

Timu ya Taifa ya Ufaransa ilitwaa ubingwa wa Kombe la Dunia baada ya kuifunga Croatia mabao 4-2.Mbinu ya kufanya mashambulizi ya kushtukiza na uzoefu dhidi ya Croatia ni miongoni mwa silaha zilizotumika kumbeba kocha wa Ufaransa Didider Deschamps kuingia kwenye rekodi ya kutwaa Kombe la Dunia kwa nyakati tofauti akiwa kocha na mchezaji.

Deschamps aliungana na Mario Zagallo wa Brazil na Franz Beckenbauer wa Ujerumani waliowahi kupata mafanikio kama hayo.

Julai 19

Simba yamtangaza kocha mpya.

Suala la kuajiri makocha ndani ya klabu ya Simba liliendelea mwaka huu baada ya kumtangaza kocha Patrick Aussems kuwa kocha mkuu wa timu hiyo akichukua nafasi ya Mfaransa, Pierre Lechantre, Aussems raia wa Ubelgiji alipewa mkataba wa mwaka mmoja huku uongozi ukimpa sharti moja la kuhakikisha anaipa ubingwa timu hiyo.

Julai 23

Sanga ajiuzulu Yanga

Aliyekuwa makamu mwenyekiti wa Yanga, Clement Sanga alijiuzulu nafasi yake kwa madai ya kutishiwa kuuwawa.

Sanga alikuwa mjumbe wa saba wa Kamati ya Utendaji ya Yanga kujiuzulu akitanguliwa na aliyekuwa mwenyekiti Yusuph Manji, Ayoub Nyenzi, Hashim, Abdallah, Salum Mkemi na Omari Said.

Julai 26

Usajili wa Kagere, Ngassa watikisa.

Kama kuna usajili uliotikisa kwenye dirisha kubwa la usajili ni wa Meddie Kagere aliyesajiliwa Simba akitokea Gor Mahia ya Kenya.

Mshambuliaji huyo ambaye alifanya vizuri kwenye mashindano ya SportPesa yaliyofanyika Kenya Juni mwaka huu pia alikuwa akiwaniwa na Yanga kabla ya Simba kumuwahi na kumsajili.

Pia usajili wa Mrisho Ngassa’Anko’ kwenda Yanga nao ulitikisa kutokana na watu wengi kuhoji kiwango chake.

Wengi walihoji Yanga imemsajili Ngassa wa nini kwani hana ubora hivi sasa ingawa tayari ameshawathibitishia waliokuwa wakichonga kuwa yeye bado wamo yaani ana kiwango.

Katika usajili hu Yanga iliwasajili Heritier Makambo,Deus Kaseke, Nkizi, Klaus Kindoki, Feisal Salum na Jaffar Mohammed wakati Simba iliwasajili Pascal Wawa, Cletus Chama, Deogratius Munishi’Dida’, Marcel Kaheza, Adam Salamba, Mohammed Rashid na Hassan Dilunga.

Julai 30

KCB yadhamini Ligi Kuu Bara

Benki ya KCB ilitoa sh 420 milioni kwa ajili ya kudhamini Ligi Ku Tanzania Bara kwa mwaka mmoja.

Mkataba huo uliwekwa saini na Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania(TFF) ,Wallace Karia na Mkurugenzi Mtendaji wa KCB,Cosmas Kimario. Benki hiyo imeboresha udhamini kwa mwaka huu kwani mwaka jana ilitoa sh 325 milioni.

Katika udhamini huo kila klabu ilitakiwa kupata sh 15 milioni huku fedha nyingine zikitumika katika shughuli mbalimbali za uendeshaji wa ligi.



Chanzo: mwananchi.co.tz