Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

YALIYOJIRI JANUARY 2018: Athumani Juma Chama afariki dunia

32541 Juma+pic Tanzania Web Photo

Thu, 20 Dec 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Mwaka 2018 unaelekea ukingoni na kuna matukio mbalimbali yakukumbukwa katika michezo ya kufurahisha na kuhuzunisha yalitokea ndani na nje ya Tanzania.

Gazeti hili litakukumbusha baadhi ya matukio muhimu yaliyojiri ndani ya mwaka huu kuanzia Januari hadi Disemba.

Januari 3

Serikali yafuta vyama vya michezo

Serikali ilitangaza kuvifuta vyama vyote vya michezo vinavyoendesha shughuli zake bila kuwa na ofisi zinazoeleweka.

Kauli hiyo ilitolewa na Msajili wa Klabu na vyama vya michezo nchini Ibrahim Mkwawa ambaye alisema pamoja na Tanzania kuwa na vyama zaidi ya 58 asilimia kubwa vimekosa sifa kwa kutokuwa na ofisi hivyo watendaji wake kuendesha shughuli zao kwa kutumia simu za mikononi au ofisi zao za kazi walikoajiriwa, jambo lisilokubalika.

Januari 8

Chama afariki Dunia

Beki wa zamani wa Yanga na Taifa Stars, Athumani Juma Chama ‘Jogoo’ alifariki dunia katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili alikokuwa akipatiwa matibabu ya kiharusi.

Chama alipata umaarufu miaka ya 1980 akiunda ngome iliyobatizwa jina la ukuta wa Berlin, alijizolea sifa kutokana na upinzani wake mkubwa uwanjani na mshambuliaji wa Simba, Zamoyoni Mogella ‘Golden Boy’, alizikwa Januari 9 katika makaburi ya Kisutu jijini Dar es Salaam.

Januari 8

Mkude,Kichuya wamtega kocha

Wachezaji wa Simba, Shiza Kichuya, Jonas Mkude na Nicholas Gyan walimuweka njia panda kocha Maosud Djuma baada ya kuonyesha utovu wa nidhamu hadharani katika mashindano ya Kombe la Mapinduzi, walipogoma kukaa benchi na kumpa mkono kocha huyo baada ya kupumzishwa.

Wachezaji hao walikasirishwa na kitendo hicho katika mchezo waliofungwa bao 1-0 na URA ya Uganda, hivyo kususa kukaa benchi na kwenda vyumbani.

Januari 9

Simbu ajitoa Madola

Katibu Mkuu Shirikisho la Riadha Tanzania (RT),Wilhelm Gidabuday alitangaza kuwa mwanariadha mahiri nchini Alphonce Simbu atashiriki mbio za Dunia za nusu marathoni zilizofanyika Machi mwaka huu, hatakwenda kushiriki katika Michezo ya Madola.

Gidabuday alikata mzizi wa fitna baada ya kuibuka malumbano baina ya RT na Serikali kuhusu mbio atakazoshiriki mwanaridha huyo.

Januari 10

Chirwa aiangusha Yanga Kombe la Mapinduzi

Mshambuliaji Obrey Chirwa alimuingiza lawama kocha George Lwandamina kwa mashabiki wa Yanga baada ya kukosa penalti ambayo ingeivusha hadi fainali ya Kombe la Mapinduzi dhidi ya URA ya Uganda.

Mzambia huyo alikosa penalti ya tano iliyoipa ushindi URA wa 5-4 baada ya suluhu kwa dakika 90.

Mashabiki walisema Chirwa hakupaswa kucheza kwa kuwa hakuwa fiti kimchezo kutokana na kutokuwa nchini kwa kip

Januari 12

Caf yafuta posho za waamuzi

Kutokana na kuwepo kwa tatizo kubwa la rushwa kwenye soka, Shirikisho la Soka Afrika (Caf) liliamua kufuta posho za waamuzi kulipwa na vyama na mashirikisho ya soka Afrika na sasa posho hizo zitalipwa moja kwa moja na Caf yenyewe kwa waamuzi wanaochezesha mechi inazozisimamia.

Miaka ya nyuma Vyama na mashirikisho ya soka ya nchi wenyeji wa michezo walihusika kulipa posho za waamuzi pamoja na wasimamizi wa michezo wakiwemo makamisaa.

Taarifa ya Caf ilisema lengo la kufanya hivyo ni kuvipunguzia mzigo vyama na mashirikisho ya soka lakini jambo kubwa ni kupambana na rushwa.

Januari 13

Azam yatwaa Kombe la Mapinduzi

Timu ya Azam FC ilitwaa ubingwa wa Kombe la Mapinduzi baada ya kuifunga URA ya Uganda kwa penalti 4-3 baada ya kushindwa kufungana ndani ya dakika 90.

Januari 16

Watatu wa tenisi wafuzu Afrika

Wachezaji watatu wa mchezo wa tenisi Kanuti Alagwa, Ester Nankulange na Shaban Mao walifuzu mashindano ya Afrika baada ya kufanya vizuri katika mashindano ya Afrika Mashariki yaliyofanyika Nairobi, Kenya.

Januari 18

Simbu ajitoa Mumbai Marathon

Mwanaridha Alphonce Simbu alijitoa kushiriki mashindano ya Mumbai Charter Marathon yaliyokuwa yafanyike Januari 21 ili kupata muda wa kujiandaa na mbio za London Marathon.

Januari 18

Kocha mpya Simba awasili.

Kocha Mfaransa Pierre Lechantre, aliwasili nchini tayari kujiunga na Simba akichukua nafasi ya Joseph Omog raia wa Cameroon, lakini naye akatimuliwa Oktoba mwaka huu.

Januari 19

Kigogo Mtwara afungiwa maisha

Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) lilimfungia maisha kujihusisha na soka aliyekuwa msimamizi wa kituo cha Mtwara, Dunstan Mkundi, akituhumiwa kubariki ubadhirifu wa fedha.



Chanzo: mwananchi.co.tz