Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

YALIYOJIRI APRIL 2018: Zahera atua Yanga kumrithi Lwandamina

33039 Zahera+pic Tanzania Web Photo

Sun, 23 Dec 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Mwaka 2018 unaelekea ukingoni na matukio mbalimbali ya michezo ya kufurahisha na kuhuzunisha yalitokea ndani ya mwaka huu Gazeti hili linakuletea matukio mbalimbali yaliyojiri ndani ya mwezi April.

April 2

Bayi azoa tuzo Madola

mwanaridha nguli wa Tanzania,Filbert Bayi alipata tuzo ya heshima baada ya kuvunja rekodi ya dunia ya mbio za mita 1500 ambayo haijawahi kuvunjwa na yeyote kwa miaka 43 kwenye michezo ya Jumuia ya Madola.Pia alipata tuzo ya uongozi kwenye Kamati ya Olimpiki Tanzania(TOC) aliyoitumikia kwa miaka 15.

Tuzo hizo zilitolewa na Rais wa Shirikisho la Jumuiya ya Madola,Louise Martin kabla ya kuanza kwa mashindano hayo Machi mwaka huu huko Carrara Australia.

April 3

Uraia wa Mtanzania wazua balaa Madola

Mwanariadha wa mbio za miruko Anthony Tapson Mwanga aliingia katika utata wa uraia wake kabla ya mashindano ya Jumuiya ya Madola yaliyokuwa yanafanyika Carrara Australia Machi kwaka huu.

Mwanga aliingia katika utata wa uraia kati ya Tanzania na Afrika Kusini jambo lililofanya Shirikisho la Riadha la Kimataifa kuzuia kibali chake kwa muda.

April 6

Mfaume atwaa ubingwa wa A. Mashariki

Bondia Mfaume Mfaume alitwaa mkanda wa ubingwa wa Afrika Mashariki na Kati baada ya kumtwanga mpinzani wake mkubwa Habibu Pengo katika pambano kali lililovuta hisisa za mashabiki wengi wa ngumu hapa nchini.

Pambano hilo lililokuwa la raundi 10 uzito wa kilogramu 66 lilifanyika kwenye Uwanja wa Kinesi Dar es Salaam.

Majaji wote watatu walimpa ushindi Mfaume wa pointi 98-92,99-91 na 99-91.

April 11

Lwandamina ajiunga na Zesco

Kocha George Lwandamina alitimka Yanga bila taarifa na ghafla akaibukia timu yake ya zamani Zesco United.

Mbinu ya kuondoka ghafla na kujiunga na timu nyingine bila kuutaarifu uongozi ndio ile ile ambayo kocha huyo alitumia wakati alipoondoka Zesco United na kujiunga na Yanga mwaka 2016.

Wakati akijiunga na Yanga huku akiwa na mkataba na Zesco aliikacha timu hiyo ya Zambia na kujiunga na Yanga kimyakimya huku akitumia mbinu ya kudanganya amekuja Tanzania kufanya shughuli zake binafsi.

Pia alivyoondoka ndani ya kikosi cha Yanga aliomba ruhusa ya kwenda Zambia kushughulikia mambo ya kifamilia lakini klabu ya Zesco ikatangaza kumchukua kocha huyo

April 17

Mchezaji tenisi atoweka Australia

Wakati ya Tanzania ilipokuwa ikijindaa kurejea kutoka kwenye mashindano ya Jumuiya ya Madola,mchezaji wa tenisi ya meza Fathiya Pazi aliingia mitini.

Mkuu wa msafara ambaye ni Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo nchini Yusuph Singo alisema alitoroka baada ya kuwategea wenzake waliokwenda kunywa chai.

Alisema walikwenda kuripoti tukio hilo polisi katika Mji wa Gold Coast lakini waliambiwa hawana uwezo wa kumkamata na kwa mujibu wa sheria za Australia mchezaji huyo hajafanya kosa.

April 18

Yanga yatinga makundi Afrika

Yanga ilitinga hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika baada ya kuitoa Welaytta Dicha ya Ethiopia kwa jumla mabao 2-1.

Licha ya kufungwa bao 1-0 katika mchezo wa marudiano uliofanyika nchini Ethiopia lakini ushindi wa mabao 2-0 waliopata nyumbani jijini Dar es Salaam uliwabeba Yanga na kufuzu hatua hiyo.

Timu hiyo ilipangwa kundi moja na Rayon Sport ya Rwanda,USM Alger(Algeria) na Gor Mahia ya Kenya.

April 22

Bao la Mbeya City laitesa Yanga

Bao la kusawazisha lililofungwa na mchezaji wa Mbeya City Iddi seleman katika mchezo dhidi ya Yanga lilizua balaa baada ya kudaiwa mchezaji mmoja aliyepewa kadi nyekundu alirejea uwanjani kushangilia bao hilo.

Yanga iliongoza bao 1-0 muda mrefu katika mchezo uliofanyika kwenye Uwanja wa Sokoine Mbeya lakini Seleman aliisawazishia Mbeya City dakika za mwisho na kuibua shangwe uwanjani hapo.

Hata hivyo Yanga kupitia kwa Mwenyekiti wa Kamati ya mashindano ya klabu hiyo Hussein Nyika waliwasilisha malalamiko katika kamati ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi(Kamati saa 72) wakidai kuwa mchezaji alipewa kadi nyekundu lakini alirejea uwanjani kushangilia bao hilo na wenzake jambo ambalo ni makosa.

April 23

Yanga yamleta kocha mpya

Yanga ilimleta kocha Mwinyi Zahera kuchukua nafasi ya George Lwandamina aliyetimkia kwao Zambia.

Zahera ni kocha msaidizi wa timu ya Taifa ya DR Congo na baada ya kuwasili Dar es Salaam kesho yake alipelekwa katika kambi ya Yanga iliyokuwa Morogoro ikijindaa na mchezo wa watani wa jadi dhidi ya Simba.

Aprili 30

Serengeti Boys mabingwa Cecafa

Timu ya vijana chini ya miaka 17 ’Serengeti Boys’ ilitwaa ubingwa wa Afrika Mashariki na Kati(Cecafa) baada ya kuichapa Somalia mabao 2-0.Serengeti Boys ilitinga fainali baada ya kuifunga Kenya mabao 2-1.



Chanzo: mwananchi.co.tz