Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wolff, Hamilton wapongezwa kwa uungwana

Max 3 696x392 Max Vestarppen akiwa mbele ya Lewis Hamilton

Tue, 14 Dec 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Bingwa wa dunia wa Formula 1 2021, Max Verstappen amefunguka kwamba alipokea ujumbe wa pongezi kutoka kwa bosi wa timu ya Mercedes Toto Wolff kufuatia mbio za Jumapili wa Abu Dhabi Grand Prix.

Verstappen mwenye umri wa miaka 24, alinufaika na gari la usalama la mbio na kumpita Hamilton katika mzunguko wa mwisho kabisa wa msimu uliyokuwa na mabo mengi na kutwaa taji lake la kwanza la dunia na kuwabania Mercedes na Hamilton rekodi ya nane.

Ingawa Mercedes wamekata rufaa juu ya tafsiri ya ubunifu ya FIA ya sheria ili kuhakikisha mbio za mwisho, Wolff na Hamilton wote walikuwa na huruma kwa Red Bull ambao hawakushiriki katika mabishano hayo.

“Toto alinitumia ujumbe wa kunipongeza kwa msimu huu, nilistahili kushinda,” Verstappen alisema. “Hiyo ilikuwa nzuri kwake bila shaka, hisia zilipanda sana kupitia mzunguko huo wa mwisho kutoka pande zote za timu zote mbili.”

“Lewis amekuwa mwanamichezo mzuri kwa ujumla. Alinijia, akanipongeza na lazima ilikuwa ngumu sana katika mzunguko huo wa mwisho. Pia inaonyesha heshima tuliyokuwa nayo kwa kila mmoja, kwa ujumla,” aliongeza Verstappen.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live