Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wimbledon kuchangia Shilingi Bilioni Moja

IMG 3939.png Wimbledon kuchangia Shilingi Bilioni Moja

Fri, 28 Apr 2023 Chanzo: Dar24

Wimbledon wanajiandaa kuchangia kiasi cha zaidi ya Pauni-500,000 (sawa na Sh bilioni 1) kwa Ukraine baada ya “uamuzi mgumu” wa kuondoa kifungo kwa wachezaji wa Urusi na wale wa Belarus.

Klabu za England (AELTC) na Chama cha Tenisi (LTA) pia zitachangia mfuko huo kwa kugharamia malazi ya wachezaji wa Ukraine watakaoshiriki mashindano hayo.

Wachezaji wa Urusi na wale, wa Belarus hawakuruhusiwa kushiriki mashindano ya mwaka jana wakijibu uvamizi wa Urusi dhidi ya Ukraine. Mwenyekiti Ian Hewitt amesema kuondoa vikwazo hakupunguzi tatizo la uvamizi.

Wimbledon na Shirikisho la mchezo wa tenisi la Uingereza na TTA waliadhibiwa na WTA na ATP kutokana na msimamo wao na walipunguzwa pointi na kuondolewa kwa kifungo hicho mwezi uliopita.

“Huu ni uamuzi mgumu sana kufikiwa, Kibinafsi nasema kuwa naona kama uamuzi mgumu zaidi kufanyika wakati wa kipindi cha uenyekiti wangu,” amesema Hewitt, ambaye atamaliza muda wake mwishoni mwa mashindano ya mwaka huu.

Akizungumzia hatua kadhaa zilizochukuliwa kuhusu misaada ya fedha kuunga mkono wachezaji wa Ukraine, Hewitt amesema kila pauni moja katika kila tiketi itachangia katika msaada wa Ukraine, ambayo ni zaidi ya Pauni 500,000.

Pia alisema kuwa AELTC na LTA watalipia vyumba viwili vya hoteli kwa kila mchezaji wa Ukraine atakayeshiriki mashindano ya Wimbledon au mechi za kufuzu kushiriki mashindano hayo.

Wachezaji hao pia wataalikwa kufanya mazoezi Wimbledon au katika viwanja vya Surbiton wakati wa mashindano hayo, wakati wakimbizi 1,000 wa Ukraine watakaribishwa kwa siku wakati wa mashindano hayo makubwa, ambayo yatafanyika kuanzia Julai 3 hadi 16.

Warusi na wenzao wa Belarus wanaotarajia kucheza katika mashindano ya Wimbledon lazima kusaini makubaliano yanayoonesha kuwa hawataonesha ishara zozote za kuunga mkono vita au kupokea msaada wa fedha kutoka nchini kwao au kampuni zinazohusika nao.

Bendera kutoka ama nchi zao au alama za kuwasapoti nazo pia zimezuiwa, kwa mujibu wa mkataba huo.

Chanzo: Dar24