Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Waziri:Wachezaji 10 wa kigeni ruksa Ligi Kuu

68188 Wachezaji+pic

Thu, 25 Jul 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Serikali imeridhia ongezeko la wachezaji 10 wa kigeni, lakini imetoa masharti makubwa mawili ambayo yanaweza kuwa mfupa mgumu kwa klabu za Simba na Yanga.

Akizungumza Dar es Salaam jana, Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo Dk Harrison Mwakyembe, alisema kuanzia msimu ujao wa mashindano klabu itaruhusiwa kusajili mchezaji wa kigeni anayecheza katika Ligi Kuu na timu ya Taifa ya nchi yake.

Tamko hilo la Serikali linaweza kuziathiri Simba na Yanga zinazoongoza kwa kusajili idadi kubwa ya wachezaji wa kigeni ambao hawachezi timu zao za taifa.

Dk Mwakyembe alisema lengo la kuweka kanuni hiyo ni kudhibiti idadi kubwa ya wachezaji wa kigeni wanaokuja nchini kucheza soka bila ya kuwa na viwango bora.

“Karia (Wallace) alipoingia madarakani aliongeza idadi kutoka watano hadi 10 kwa kila klabu, suala ambalo limenisumbua sana bungeni,” alisema Dk Mwakymbe.

Alisema suala la wachezaji wa kigeni liliibuka bungeni kabla ya kutoa mapendekezo ya kuwe na mjadala mpana utakaohusisha wadau wa soka.

Pia Soma

“Hatutaki kila mchezaji ameibuka tu katika ndondo anakuja kucheza kwenye ligi yetu, tumeridhia idadi ya wachezaji 10 wa kigeni kwa masharti hayo,” alisema Dk Mwakyembe. Waziri huyo alisema mwaka jana wachezaji 52 wa kigeni walisajiliwa na mwaka huu 42.

“Nchi ambazo ziko juu kimpira kulinganisha na Tanzania wachezaji wake wanaocheza daraja la pili au la kwanza wataangaliwa,”alisema Karia ambaye ni rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF).

Chanzo: mwananchi.co.tz