Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Waziri Shonza aiaga Taifa Stars kupaa kesho Misri Afcon

61548 CAF+PIC Waziri Shonza aiaga Taifa Stars kupaa kesho Misri Afcon

Thu, 6 Jun 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Naibu Waziri Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo, Juliana Shonza amesisitiza nidhamu kwa wachezaji timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' kuelekea fainali za Mataifa ya Afrika 'Afcon'.

Shonza ameiaga Stars iliyowekwa kambini hoteli ya Whitesands inatarajiwa kusafiri kesho kwenda Misri wataendelea na kambi ya wiki mbili kabla ya kuanza kwa fainali hizo za Afcon.

"Nampongeza kocha Emmanuel Amunike na benchi zima la ufundi kwa kazi kubwa iliyoifanya kwa Taifa Stars kupata nafasi ya kushiriki fainali za Afcon.

"Kuna majukumu mengine makubwa mbele yenu nchini Misri, nidhamu itawabeba na niseme tu kwa niaba ya Waziri na Serikali kwa ujumla tunawatakia kila la kheri na tupo nyuma yenu," alisema waziri Shonza.

SAMATTA ATOA NENO

Akizungumza kwa niaba ya wachezaji nahodha wa Taifa Stars, Mbwana Samatta alisema anaishukuru Serikali kwa kuwaunga mkono.

Pia Soma

"Nimefurahi kula wote chakula cha mchana, tumefurahi sapoti yenu tangu katika michezo ya kuwania nafasi ya kwenda katika fainali za Afcon," alisema Samatta.

Kocha wa Taifa Stars, Emmanuel Amunike alisema kujituma kwa kila mchezaji ndiko kutakowafanya kufanya vizuri katika fainali hizo.

"Ninawachezaji wazuri ambao naamini tunaweza kufanya vizuri kikubwa ni kutobadili mtazamo tulionao kichwani wa kwenda kushindana na siyo kuahiriki," alisema Amunike.

Chanzo: mwananchi.co.tz