Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Waziri Ndumbaro, Jaji Mihayo wavishwa uzi wa Yanga

Ndumbaro Pic Data Waziri Ndumbaro, Jaji Mihayo wavishwa uzi wa Yanga

Fri, 17 Sep 2021 Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

KAMA utani Waziri wa Maliasili na Utalii, Damas Ndumbaro na Mwenyekiti wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), Jaji Thomas Mihayo ambao ni Simba damu mapema leo wamelazimika kutinga uzi wa Yanga wakati klabu hiyo kongwe ikitangaza kujitolea kujitolea kutangaza utalii kupitia Mlima Kilimanjaro na Zanzibar.

Yanga ilitangaza hatua ya kuvaa nembo yenye vivutio vya utaliiya Visit Kilimanjaro & Zanzibar kwenye jezi zao upande wa mkono wa kushotio katika mechi zao za kimataifa, bila kulipwa senti yoyote.

Hata hivyo kabla ya kutangazwa kwa hatua hiyo mbele ya wanahabari, Waziri Ndumbaro na Jaji Mihayo ambao ni Simba lialia walikabidhiwa jezi mpya za Yanga na kuzitinga huku wakitaniwa na Msemaji wa Simba, Haji Manara aliyekuwa sambamba na Kaimu Katibu Mkuu, Haji Mfikiriwa.

Waziri Ndumbaro alikaririwa wakati akitaniwa akidai kuwa amevaa uzi huo kwa vile Yanga imeamua kutangaza utalii ambayo yeye anausimamia, huku akisisitiza kuwa, Yanga ndio iliyopeleka wazo la kujitolea bure kutangaza Mlima Kilimanjaro na Zanzibar na wao wamepokea kwa furaha.

"Huwezi kutenganisha michezo na utalii, mechi za Simba na Yanga ambayo haikucheza tuliona mashabiki wengi wa kigeni wakilalamika," alisema Ndumbaro, huku Mfikirwa akisema; "Tunajua tuna mashabiki ndani na nje ya nchi, ndio maana tumetumia fursa ya mchezo wetu wa ugenini kutangaza utalii wetu."

"Matangazo yote ya kwenye jezi huwa yanalipwa, ila sisi hatujalipwa kwa vile tumefanya kwa lengo la kuitangaza nchi," ameongeza Mfikirwa.

Yanga imekuwa imejitoza kutangaza utalii ikifuata nyayo zilizofanywa na watani wao msimu uliopita katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika kwa kuitangaza Tanzania kwa ujumla kwa kuweka tangazo kifuani kwa jezi zao linalosomeka 'Visit Tanzania'.

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz