Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Waziri Mwakyembe aja na muarobaini wa migogoro ya ngumi za kulipwa

1069 MWAKYEMBE TZW

Thu, 4 Jan 2018 Chanzo: bongo5.com

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe (Mb) jana tarehe 3 Januari, 2018 amekutana na wadau wa mchezo wa ngumi za kulipwa nchini. Kikao hicho ni mwendelezo wa vikao vya Mhe. Waziri na Wadau hao ili kutatua migogoro iliyodumu kwa muda mrefu katika mchezo huo wa masumbwi ya kulipwa, vikao hivyo vilianza mwishoni mwa mwaka 2017. 

TAARIFA KWA UMMA

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe (Mb) leo tarehe 3 Januari, 2018 amekutana na wadau wa mchezo wa ngumi za kulipwa nchini. Kikao hicho ni mwendelezo wa vikao vya Mhe. Waziri na Wadau hao ili kutatua migogoro iliyodumu kwa muda mrefu katika mchezo huo wa masumbwi ya kulipwa, vikao hivyo vilianza mwishoni mwa mwaka 2017. Katika kikao kilichofanyika leo, Mhe. Waziri aliwaagiza wadau hao kufanya kazi kwa pamoja katika kuunda mfumo mpya utakaolinda maslahi ya mabondia na wahusika wengine wa mchezo wa ngumi za kulipwa na kuliletea Taifa letu heshima kwa kupitia mchezo huo kama ilivyokuwa miaka ya nyuma.

Ili kupiga hatua, Waziri Mwakyembe ameunda kamati ya watu kumi na moja (11) itakayokusanya maoni ya wadau na kupitia upya katiba ya kuunda Chombo kitakachosimamia mchezo wa ngumi za kulipwa hapa nchini. Kamati hiyo imeanza kufanya kazi leo  tarehe  03 Januari, 2018 na itakamilisha kazi yake tarehe 31 Januari, 2018. Kamati itasimamiwa na Baraza la Michezo la Taifa (BMT) na itakuwa na wajumbe wafuatao:-:

Ndg. Emmanueli Salehe         –     Mwenyekiti Ndg. Joe Enea                      –     Makamu Mwenyekiti Ndg. Yahya Pori                    –     Katibu Ndg. Habibu A. Nyogoli         –     Mjumbe Ndg. Shomari Kimbau           –     Mjumbe Ndg. Fike Wilson                  –     Mjumbe Ndg. Anthony Ruta               –     Mjumbe Dkt. Killaga M.Killaga           –     Mjumbe Ndg. Ally B. Champion         –     Mjumbe Ndg. Rashidi Matumla          –     Mjumbe Ndg. Karama Nyilawila         –    Mjumbe Aidha, Waziri Mwakyembe ameeleza kwamba katika kipindi cha mpito shughuli za kutoa vibali kwa mapambano ya ndani na kwa mabondia wanaosafiri nje ya nchi zitaendelea kutekelezwa na BMT. “BMT endeleeni kusimamia vibali vya mapambano ya ndani na vibali vya safari za nje ya nchi za mabondia kwa kuzingatia uzalendo, weledi, kanuni na sheria za nchi bila kumwangalia mtu usoni wala kumuonea aya”, amesisitiza Waziri Mwakyembe.

 

Imetolewa na

 

Octavian F. Kimario

Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini,

Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo.

03/01/2018

Chanzo: bongo5.com