Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Waziri Mkuu aagiza Dodoma FC ikabidhiwe Jiji

Mon, 22 Oct 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dodoma.Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ameagiza timu ya Dodoma Football Club (DFC) ikabidhiwe kwa uongozi wa Jiji ili waiendeshe.

Ameagiza viongozi wote wa mkoa kuhakikisha wanapambana ili timu hiyo ipande na kucheza ligi kuu msimu ujao.

Majaliwa amesema ni aibu kubwa mkoa wenye makao makuu kutokuwa na timu za maana halafu Jiji wanasema kuwa wanakusanya vizuri.

Akizungumza na wakazi na watumishi wa Jiji, Jana, Majaliwa alisema inamkera kuona Dodoma haina timu kubwa na iliyopo haiungwi mkono.

"Mkurugenzi mnashindwaje kuichukua DFC ambayo inafanya vizuri, na kwa taarifa yenu jana (juzi) ilimpiga mtu 2-1 kule Dar es Salaam, nataka muichukue na muendeleze vipaji na kuzalisha timu zingine," alisema Majaliwa.

Mkurugenzi wa Jiji Godwin Kunambi alikubali kuichukua timu hiyo ikiwa wadau wataruhusu ichukuliwe na Jiji.

 

Chanzo: mwananchi.co.tz