Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Waziri: Klabu ziige uwekezaji Simba

Bashungwa ED Waziri: Klabu ziige uwekezaji Simba

Mon, 26 Apr 2021 Chanzo: ippmedia.com

Bashungwa alitoa pongezi hizo juzi alipotembelea Mradi wa Ujenzi wa Kituo cha Michezo cha Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), ulioko Kigamboni, jijini Dar es Salaam.

"Ninazikaribisha klabu zingine kushirikiana na serikali ili kuendana na Dira ya Serikali na maelekezo ya Rais wetu, Samia Suluhu Hassan, ya kutaka sekta hii kutoa ajira kubwa kwa vijana na kuchangia kwenye pato la nchi," alisema.

Bashungwa pia alitumia nafasi hiyo kuipongeza Simba kwa kufika hatua ya robo fainali katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika, huku akiwataka Watanzania kuonyesha uzalendo kwa kuiunga mkono klabu hiyo inayoitangaza Tanzania kimataifa na kupitia kauli mbiu yao ya Visit Tanzania (Tembelea Tanzania) katika jezi zao.

Katika ziara yake hiyo, waziri huyo alikagua mradi huo unaofadhiliwa na Shirikisho la Soka la Duniani (FIFA), akishuhudia shughuli za ujenzi zikiendelea na kujiridhisha na kutoa rai kwa uongozi kufanikisha ujenzi wa viwanja vinne kufikia mwishoni mwa mwaka huu.

Rais wa TFF, Wallace Karia, alibainisha huduma za kimichezo zitakazokuwa zinapatikana kwenye mradi huo unaotekelezwa Dar es Salaam na Tanga, kuwa ni mpira wa miguu kwa viwanja vya nyasi bandia na za kawaida, hoteli ya hadhi ya nyota tatu, hosteli kwa wakufunzi wanamichezo, viwanja vya mpira wa wavu na pete na mabwawa ya kuogelea.

Chanzo: ippmedia.com