Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Waziri Gekul asisitiza wadau kuunga mkono michezo

Waziri Gekul Asisitiza Wadau Kuunga Mkono Michezo Waziri Gekul asisitiza wadau kuunga mkono michezo

Sun, 25 Dec 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Pauline Gekul Desemba 23, 2022 wilayani Rombo Mkoa wa Kilimanjaro, amezindua mbio za Rombo Marathon zilizoandaliwa na Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia ambaye pia ni Mbunge wa Rombo, Mhe. Prof. Adolf Mkenda.

Akizungumza baada ya kuzindua mbio hizo ambazo ameshiriki kukimbia kwa urefu wa KM 10, Mhe. Gekul amesisitiza wadau kujitokeza kuunga mkono shughuli za michezo ili kuhamasisha Wananchi wengi kushiriki michezo.

Kwa niaba ya Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Mohamed Mchengerwa, nakupongeza Waziri na Mbunge wa Rombo kwa kuanzisha Marathon hii ambayo inaunga mkono Sera ya Michezo na kutoa nafasi kwa wananchi kuongeza kipato chao", amesema Mhe. Gekul

Kwa upande wake Waziri na Mbunge wa Rombo, Mhe. Prof. Adolf Mkenda amesema lengo la Marathon hiyo ni kutangaza Utalii uliopo katika Wilaya ya Rombo, kuwaunganisha wananchi wa mkoa huo na mikoa jirani hasa kipindi hiki ambacho wananchi wengi wanakusanyika kushereheka sikukuu, huku akisisitiza kuwa Marathon hiyo itakua endelevu na kufanyika kila mwezi Desemba.

Marathon hiyo imeshirikisha mbio zenye urefu wa KM 21, 10 na 5 kwa wanaume, wanawake pamoja na wenye ulemavu ambapo michezo mingine kama kuvuta kamba, kukimbiza kuku na mengine, huku Wasanii mbalimbali wa muziki wa kizazi kipya wa zamani wakitoa burudani.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live