Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Innocent Bashungwa amesema pindi vilabu vyetu vikiwa vinawakilisha nchi Kimataifa basi tuache ushabiki na kuziunga mkono ili ziendelee kufanya vema.
Waziri Bashungwa amesema, "Tuondoe ushabiki wetu na kusapoti timu zetu zinapowakilisha nchi, umoja tulioonesha kwa timu zetu za Taifa ikiwemo Taifa Stars basi umoja huo uonyeshwe katika klabu zetu zinapowakilisha Taifa"
Maneno hayo yamelenga kuwataka wafuasi wa soka nchini kuiunga mkono kwa maana ya kuishangilia Simba SC itakapocheza na Red Arrows ya Zambia Jumapili ya kesho Novemba 28, 2021 kwenye dimba la Benjamin Mkapa ukiwa ni mchezo wa mtoano kuwania kufuzu hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Arika.