Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Watu sita wapotea wakicheza Skiing

Skiing Alps Watu sita wapotea wakicheza Skiing

Mon, 11 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Waokoaji nchini Uswizi wanawatafuta watu 6 ambao wamepotea katika Milima ya Alps walipokuwa wakifanya mchezo wa kuteleza juu ya theluji (Skiing).

Watu hao, watano wakiwa wa familia moja walipotea siku ya Jumamosi karibu na Mlima wa Matterhorn.

Hali ya hewa Milimani humo ni mbaya inayoambatana na kimbunga, pamoja na hatari ya kuangukiwa na wingi wa theluji.

Hali hii imezuia hata helikopta kufika kwenye maeneo hayo ili kuongeza nguvu kwenye zoezi la utafutaji. Waliopotea wana umri kati ya miaka 21 na 58.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live