Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Watatu wachukua fomu kuwania Urais TFF

KARIA Watatu wachukua fomu kuwania Urais TFF

Wed, 9 Jun 2021 Chanzo: eatv.tv

Wanafamilia watatu wa mpira wa miguu wamejitokeza kuchukua fomu za kuwania nafasi ya Urais wa shirikisho la mpira wa miguu Tanzania (TFF), miongoni mwa waliochukua fomu ni pamaoja na Rais wa sasa Wallace Karia.

Submitted by Ibra Kasuga on Jumatano , 9th Jun , 2021 Rais wa sasa wa TFF Wallace Karia

Waliochukua fomu mpaka sasa ni Evans G. Mgeusa, Zahor Mohammed Haji na Rais aliyekuwepo madarakani Wallace Karia ambaye anatetea nafasi yake wote hawa wanawania nafasi ya Rais. Zoezi la uchukuaji fomu za kugombea nafasi za uongozi TFF lilianza hapo jana Juni 8, 2021 na litadumu mpaka Juni 12, 2021, Saa 10:00 Jioni.

Uchaguzi mkuu wa kuchagua viongozi wa TFF utafanyika Agosti 7, 2021 huko mkoani Tanga. Na nafasi zinazowaniwa ni Nfasi moja ya Rais na nafasi sita za Wajumbe wa Kamati ya Utendaji.

 

Chanzo: eatv.tv