Michuano ya Pool table ya Grand Mchana Open Festival yaliyofanyika nchini Kenya yamemalizika na Watanzania wawili wakifanya vizuri katika michuano hiyo.
Mtanzania Seif Hamad amekuwa mshindi wa pili katika michuano hiyo na kuondoka na kitita cha Sh6 milioni huku mtanzania Festo Yohana yeye akishika nafasi ya tatu na kuondoka na Sh3.7 milioni.
Mshindi wa kwanza wa michuano hiyo ni Ibra Ssejemba raia wa Uganda aliyeondoka na kitita Cha Sh12.5 milioni.
Michuano hiyo ilihusisha nchi 8 za Afrika ambazo ni Tanzania, Zambia, Afrika Kusini, Zimbabwe, Sudan, Kusini, Somalia, Kenya, na Uganda ikiwa na washiriki 128.
Watanzania hao wataungana na timu ya Taifa ya pool table nchini kwenda kushiriki michuano ya Afrika yatakayofanyika nchini Afrika Kusini kuanzia Oktoba 11.