Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Washambuliaji Serengeti Boys mzuka AFCON

49545 PIC+SERENGETI

Mon, 1 Apr 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. ZIKIWA zimebaki siku 15 kuelekea fainali za Mataifa ya Afrika kwa vijana (AFCON U17), hamasa imeongezeka kwa timu ya Tanzania, Serengeti Boys, ambayo iko kambini Rwanda.

Nyota wa timu hiyo ya taifa ya vijana, wameeleza matumaini yao katika kulibakisha kombe hilo nyumbani, huku kumaliza katika nafasi mbili za juu kukitosha kufuzu kucheza Kombe la Dunia kwa vijana litakalofanyika Oktoba nchini Brazil.

Mwananchi imezungumza na baadhi ya wachezaji wanaounda kikosi hicho ambao wameelezea namna walivyojipanga.

Mmoja wa washambuliaji tegemeo wa Serengeti Boys, Agiri Ngoda (17), amesema maandalizi mazito wanayofanya na sapoti ambayo wamekuwa wakipata kutoka kila kona vinawapa hamasa ya kufanya vizuri katika michuano hiyo.

“Kikubwa tunamuomba Mwenyezi Mungu atufikishe salama kwenye mashindano, tunafahamu kila timu inahitaji ushindi, ila tumejipanga, lazima kombe libaki nyumbani,” anasema.

Anasema timu yao kila mchezaji ana ubora katika nafasi anayocheza na anaamini kwa umoja wao, msimu huu ni zamu ya Tanzania kucheza Kombe la Dunia .

Straika mwingine wa Serengeti, Salum Ally (16), amesema benchi la ufundi la timu hiyo na Shirikisho la Soka (TFF) wamefanya kazi kubwa katika kuwaandaa kwa ajili ya mashindano hayo hivyo hawatowaangusha na wataendeleza furaha ya Watanzania iliyopo hivi sasa katika michezo.

Yassin Mgaza (16), straika mwingine wa Serengeti Boys, alisema wamedhamiria kuweka rekodi mwaka huu.

“Hii ni nafasi adimu kutokea, hivyo hatupaswi kuipoteza kizembe. Hapa tulipo tunalichungulia Kombe la Dunia, siyo jambo dogo, hivyo ni lazima tupambane kwa uwezo wetu wote.”



Chanzo: mwananchi.co.tz