Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Warundi huwaambii kitu Ligi Kuu Bara

Warundi Pic Data Warundi huwaambii kitu Ligi Kuu Bara

Wed, 17 Nov 2021 Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

WAKATI mashabiki wengi wa soka nchini wakilalamikia Ligi Kuu Bara (TPL) kutokuwa na ubora unaostahili, lakini unambiwa nchi jirani ikiwemo Burundi hauwaambii kitu kuhusu ligi hiyo kwani wanaamini ni sehemu sahihi ya kutoboa huko kwao.

Kuthibitisha hilo ni jinsi nyota wawili wa timu ya taifa ya Burundi wanaocheza nchini, Bigirimana Blaise (Namungo) na Sadio Ntibazinkiza (Yanga) kutupia kambani wakati wakiisaidia timu yao kuifumua Myanmar kwa mabao 2-1 katika mchezo wa kirafiki wa kimataifa.

Moja ya mchambuzi wa soka wa Burundi, Jimmie Ndayishimiye aliliambia Mwanaspoti wachezaji wengi wa taifa hilo wanapenda kuja Tanzania kutokana na maslahi na ubora wa Ligi ya Bongo.

“Tanzania imekuwa na Ligi bBora kwa zaidi kwa Ukanda wa Afrika Mashariki na kila mchezaji kutoka maeneo haya anatamani kucheza hapo,” alisema Ndayishimiye na kuongeza;

Huko (Tanzania), wanalipa vizuri pia ligi inamvuto na ushindani mkubwa vikichagizwa na kufuatiliwa na watu wengi Afrika hususani timu za Simba na Yanga hivyo wachezaji wengi kutoka Burundi wanavutiwa na hilo kwani mara nyingi huwa kama daraja kwao.”

Naye nyota wa zamani wa Namungo anayekipuiga kwa sasa Mtibwa Sugar, Styve Nzigamasabo ambaye pia anaichezea Intamba mu Rugamba alieleza sababu za wao kupenda kucheza Tanzania.

“Ligi ya Burundi kwa sasa imepooza sana, hivyo wachezaji hawapati fursa ya kuonekana na kuweza kutimiza ndoto zao kama ilivyo Tanzania, ambapo ligi yake ni bora, ina ushindani na miundombinu bora zaidi, nadhani hizo ndio sababu wengi huja Tanzania,” alisema Steve ndugu wa damu wa Saido.

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz