Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wapigakura TFF wanyang'anywa simu

Simupic Data Wapigakura TFF wanyang'anywa simu

Sat, 7 Aug 2021 Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

Mwenyekiti wa uchaguzi wa TFF, Kiomoni Kibamba ametaka simu za wapigakura zikusanywe na zizimwe wakati wa kupiga kura.

Hata hivyo uamuzi huo uliibua minong'ono ya wapigakura huku mmoja akiomba simu zao ziwekwe kwenye meza ya mwenyekiti huyo wa uchaguzi na mpigakura akimaliza kupiga kura anaipitia.

"Nimekubali ushauri, hata kama una simu 10 tutakusachi hapa, hatutaki yatokee kama ya 2017.

"Tuna uzoefu na simu, ili jambo si geni, tulikuwa na taarifa, ukipiga kura unaipiga picha unakwenda kumuonyesha mgombea uliyempigia ndipo anakupa mzigo.

"Hili jambo si geni, sitaki maswali na hakuna kuingia na simu kwenye eneo la kupigia kura," amesema.

Amesema hata kalamu za kutumia ziko eneo la kupigia kura na ni za bluu, kura itakayopigwa na kalamu tofauti itakuwa batili.

Katika hatua nyingine, Rais wa Simba, Murtaza Mangungu amewasili kwenye uchaguzi huo na atashiriki katika kupiga kura ya kuwachagua wajumbe wa kamati ya utendaji.

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz