Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Waogeleaji Tanzania wavuna medali Afrika

Tue, 20 Nov 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

 

S. Timu ya Taifa ya kuogelea imeshika nafasi ya tatu katika mashindano ya Afrika ya Cana Kanda ya Tatu yaliyomalizika wiki iliyopita mjini Khartoum, Sudan. Tanzania imesh

Dar es Salaam.Waogeleaji wa timu ya Taifa, wamEtwaa nafasi ya tatu kwenye mashindano ya Afrika ya Cana Kanda ya Tatu yaliyomalizika Jumamosi jioni mjini Khartoum, Sudan.

Tanzania ilishika nafasi ya tatu baada ya kupata pointi 1,125, huku ikishuhudia wenyeji Sudan ikitawazwa kuwa bingwa mpya wa taji hilo baada ya kuvuna pointi 1,548 ikifuatiwa na Afrika Kusini ambayo ilitwaa pointi 1,248.

Tanzania iliyokuwa bingwa misimu miwili mfululizo tangu 2016, imeshindwa kutetea ubingwa huo nchini Sudan baada ya kuwa na idadi ndogo ya waogeleaji wa kike, ikiwakilishwa na muogeleaji mmoja wa kike.

"Tulikuwa na muogeleaji mmoja wa kike ambaye alipata pointi 92 peke yake, alifanya vizuri sana lakini wenzetu walikuwa na idadi kubwa hivyo kuongeza pointi ," alisema mwenyekiti wa Chama cha Kuogelea Tanzania (TSA), Imani Dominic.

Alisema katika matokeo ya wavulana, Tanzania ilitwaa ubingwa lakini ikaachwa na Sudan kwenye matokeo ya jumla ambapo iliambulia nafasi ya tatu.

"Kama tungekuwa na waogeleaji wa kike watano, bila shaka tungetetea ubingwa wetu kwa mara ya tatu mfululizo, lakini hatukuwa nao kwa sababu zilizokuwa nje ya uwezo wetu," alisema.

Katika mashindano hayo, Tanzania iliwakilishwa na waogeleaji 11, huku wavulana wakiwa 10 ambao walikusanya pointi 1,033 na muogeleaji pekee wa kike, Maria Bachmann akiondoka na pointi 92.

Waogeleaji wengine walioshiriki mashindano hayo ni Khaleed Ladha, Carter Helsby, Aravind Raghavindra, Mohameduwais Abdullatif, Peter Itatiro, Christopher Fitzpatrick, Delhem Mohamed, Aaron Akwenda, Yuki Omori na Christian Shirima.



Chanzo: mwananchi.co.tz