Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wanariadha waandamana kisa mauaji

Screenshot 2021 10 23 At 09.png Wanariadha waandamana kisa mauaji

Sat, 23 Oct 2021 Chanzo: Kenya24

Faith Kipyegon, Joyciline Jepkosgei, Eunice Sum na Mary Keitany ni miongoni mwa watu 300 walioandamana nyuma ya bango lililosema:‘Malizeni ukatili wa kijinsia’. Wanariadha maarufu akiwemo Eliud kipchoge , Julius Yego na Conseslus Kipruto pia walihudhuria.

Aliyekuwa mwanariadha na mshindi wa mashindano ya kimataifa wa Kenya Bi Tirop alidungwa kisu nyumbani kwake mapema mwezi huu na Maafisa wa Polisi wanamshikilia mume wake Ibrahim Rotich jela kama mshukiwa mkuu.

Mauaji ya Bi Tirop yamezua hisia kali miongoni mwa wanariadha wa Kenya kuhusu kile wanachopita inapokuja suala la ghasia za kinyumbani, jambo lililopelekea wao kuandamana wakiwa wamebeba bango kubwa kufikisha ujumbe kwa jamii juu ya jambo hilo.

Mume wa Tirop anashikiliwa kwa siku 20 sasa, ambapo atachunguzwa kubaini iwapo hali yake ya kiakili iko timamu ili kukabiliwa na mashtaka.

Chanzo: Kenya24