Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wambura aendelea kusota rumande

44415 Pic+wambura Wambura aendelea kusota rumande

Sun, 3 Mar 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam.Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, imeutaka upande wa mashitaka, katika kesi ya utakatishaji fedha inayomkabili aliyekuwa Makamu wa Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania(TFF), Michael Wambura, kukamilisha upelelezi kwa wakati.

Kauli hiyo ilitolewa jana na Hakimu Mfawidhi wa mahakama hiyo, Kelvin Mhina, baada ya upande wa mashitaka kueleza mahakama hiyo kuwa upelelezi wa shauri hilo bado haujakamilika.

“ Nataka tarehe ijayo upande wa mashitaka mje muiambie mahakama upelelezi wa kesi hii umefikia hatua gani” alisema Hakimu Mhina.

Awali, Wakili wa Serikali Wankyo Simon alidai kesi hiyo imekuja kwa ajili ya kutajwa na upelelezi wa shauri bado haujakamilika. “Shauri limekuja kwa ajili ya kutajwa na upelelezi bado haujakamilika, hivyo tunaomba tarehe nyingine kwa ajili ya kutajwa”alidai Simon.

Baada ya Simon kueleza hayo, Majura Magafu, ambaye ni Wakili wa mishtakiwa, aliutaka upande wa mashtaka ujitahidi kukamilisha upelelezi kwa wakati.

Hakimu Mhina, baada ya kusikiliza maelezo ya pande zote aliahirisha kesi hiyo hadi Machi 14, 2019 kesi hiyo itakapotajwa. Mshtakiwa wamerudishwa rumande kutokana na mashtaka yanayomkabili kutokuwa na dhamana.

Wambura alifikishwa Kisutu kwa mara ya kwanza, Februari 11, mwaka huu, akikabiliwa na mashtaka 17 yakiwemo ya kutakatisha fedha zaidi ya Sh 100milioni, katika kesi ya uhujumu uchumi namba 10/2019.



Chanzo: mwananchi.co.tz