Nahodha wa Simba John Bocco amechaguliwa kuwa mchezaji bora wa Ligi Kuu Tanzania Bara 2020-21 akiwashinda Mukoko Tonombe (Yanga) na Clatous Chama (Simba). Utoaji wa tuzo hizo umefanyika Oktoba 21 jijini Dar es Salaam mbele ya Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa. Hizi ndiyo tuzo zote pamoja na vikosi bora vya msimu,
1. Mshambuliaji wa Namungo, Reliants Lusajo ametwaa tuzo ya mfungaji bora wa Kombe la Shirikisho la Azam (ASFC). Lusajo katika michuano hiyo alifunga mabao manne na tuzo yake imepokelewa na mtendaji mkuu wa Namungo, Omari.
2. Ruvuma Queens imechukua tuzo ya timu yenye nidhamu Ligi Kuu ya Wanawake (SWPL)
3. Nahodha wa Simba, John Bocco amepata Tuzo ya mfungaji bora wa Ligi Kuu Bara msimu wa 2020/2021. Katika msimu huo Bocco alifunga jumla ya mabao 16.
4. Timu ya Coastal Union imeshinda tuzo ya timu yenye nidhamu ikizifunika Mwadui na Simba.
5. Meneja wa Uwanja wa Nelson Mandela uliopo Sumbawanga, John Zwala ameibuka Meneja Bora wa Uwanja kwa msimu wa 2020/2021.
John amewashinda Sikitu Kitakala (Azam Complex, Dar), na Midestus Mwalukwa (Sokoine, Mbeya).
6. Kamishina wa mechi, Pili Mlima kutoka Arusha ameshinda tuzo ya tuzo Kamishina bora wa mechi
7. Seti bora ya Waamuzi wa msimu uliopita ni ile iliyochezesha mechi kati ya Simba na Mtibwa Sugar kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa.
Waamuzi hao ni Ahmed Arajiga, Reonard Mkumbo, Hamdani Said na Hellen Mduma.
8. Sikudhan Mkulungwa, amepata tuzo ya mwamuzi bora msaidizi kwa Ligi Kuu ya Wanawake
9. Amina Kyando Mwamuzi Bora Ligi ya Wanawake Tanzania akiwashinda Tatu Malongo na Esther Adabert.
10. Frank Komba Mwamuzi bora msaidizi wa Ligi Kuu Bara na amewashinda Ramadhan Kayoko na Emannuel Mwandemwa.
11. Aliyekuwa Kocha Mkuu wa Yanga Princess, Edina Lema ameibuka kuwa Kocha bora wa Ligi ya Wanawake akiwashindaMussa Mgosi (Simba Quees) na Ally Mohamed (JKT Queens).
12. Bongo Zozo muhamasishaji Bora. Bongo amewashinda Masau Bwire (Ruvu Shooting) na Haji Manara (Simba, ambaye kwa sasa ni msemaji wa Yanga).
13. Mchezaji wa Alliance Queens, Asha Juma ameshinda tuzo ya mchezaji bora Chipukizi Ligi ya Wanawake.
Asha amewashinda Husnath Ubamba (Fountain Gate) na Hadija Petro (TSC)
14. Abdul Seleman ‘Sopu’ mchezaji bora chipukizi.
Sopu anayechezea Coastal Union amewashinda Deogratius Judika (Biashara United) na Lusajo Mwaikenda (KMC/Azam)
15. Golikipa wa Simba, Aishi Manula ameibuka kipa bora wa Kombe la Shirikisho (ASFC) kwa msimu uliopita.
Manula amewashinda Faruk Shikhalo (Yanga sasa KMC) na James Ssetuba (Biashara United)
16. Janeth Shija ameshinda tuzo ya kipa Bora Ligi ya Wanawake.
Janeth amewashinda Husna Zuberi (Yanga Princess) na Najiath Abbas (JKT Queens).
17. Aishi Manula amechukua tuzo ya Golikipa Bora wa Ligi Kuu Bara.
Manula amewashinda Jeremiah Kisubi (Tanzania Prisons sasa Simba) na Harun Mandanda (Mbeya City).
18. Beki wa kushoto wa Simba, Mohamed Hussein ‘Tshabalala’ amepata tuzo ya beki bora.
Tshabalala amewashinda Dickson Job (Yanga) na Shomari Kapombe (Simba).
19. Aliyekuwa kiungo wa Simba, Clatous Chama ameibuka kiungo bora wa Ligi Kuu Bara. Chama amewashinda Feisal Salum na Mukoko Tonombe wote wa Yanga.
20. Kibwana Shomari wa Yanga ameshinda Tuzo ya mchezo wa kiungwana ‘Fair Play’. Tuzo hiyo ilikuwa ni maalumu.
21. Ramadhan Kayoko amechukua tuzo ya Mwamuzi Bora wa Ligi Kuu Bara kwa msimu uliopita.
Kayoko amewashinda Emannuel Mwandembwa na Ahmed Arajiga.
22. Marehemu Maneno Tamba amepewa Tuzo ya heshima kwa soka la wanawake nchini. Tuzo hiyo imepokelewa na mkewe.
23. Lambart Sabiyanka amechukua tuzo ya goli (bao) bora la Ligi Kuu kwa msimu uliopita.
Lambart aliifungia bao hilo timu yake (Tanzania Prisons) kwenye mechi dhidi ya Mwadui Novemba 29, 2020. Katika tuzo hiyo alikuwa akiwania dhidi ya Bernard Morrison, Mohamed Hussein, Prince Dube, Stephen Sey na Feisal Salum.
24. Amina Bilali wa Yanga Princess ameshinda Tuzo ya Mchezaji Bora Ligi Kuu ya Wanawake akiwashinda Opah Clement (Simba) na Aisha Masaka (Yanga)
25. Feisal Sakum 'Feitoto' wa Yanga amechukua Tuzo ya mchezaji bora wa Kombe la Shirikisho la Azam (ASFC).
Feisal amewashinda Luis Miquissone na John Bocco wote wa Simba.
26. Tuzo maalumu ya Raisi wa TFF, Wallace Karia imekwenda kwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa.
27. Tuzo ya Mchezaji Gwiji imetolewa kwa mchezaji wa zamani wa Simba, Abdallah King Kibaden
28. Kikosi bora cha Ligi ya Wanawake;
1. Janeth Shija 2. Julieth Singano 3. Happy Hezron 4. Vaileth Nicholas 5. Fatuma Issa 6. Amina Bilali 7. Stumai Abdallah 8. Opa Clement 9. Aisha Masaka 10. Mawete Mussolo.
29. Kikosi bora cha Ligi ya Wanaume;
1. Aishi Manula 2. Shomari Kapombe 3. Mohamed Hussein 4. Joash Onyango 5. Dickson Job 6. Mukoko Tonombe 7. Clatous Chama 8. Feisal Salum 9 . John Bocco
10. Prince Dube 11. Luis Miquissone.