Mshambuliaji wa zamani wa Taifa Stars, Simba na Yanga, Edibily Jonas Lunyamila amesema ugumu wa mechi za Kundi D, Ligi ya Mabingwa Afrika ilikuwa kosa kuidharau Simba au JS Saoura.
Lunyamila amesema kuwa Simba ilipoanza kwa kuilaza timu hiyo ya Algeria mabao 3-0 ikafungwa mabao 5-0 na Al Ahly kila mmoja akaona Simba haina kitu.
Kila timu imeongoza kundi hilo isipokuwa AS Vita kwamba kila hatua moja hakuna timu iliyotulia kwa muda mrefu katika kundi hilo kwenye nafasi ya kwanza ukiondoa AS Vita.
"Sasa ninachokiona, Simba ina nafasi, kila timu ina nafasi kinachosubiriwa ni jinsi watakavyozichanga karata zao, sasa huwezi kusema kundi la kubeza au timu ya kubeza. Hili kundi liko tight," alisema.
Amesema kwa ugumu huo ndio maana mashabiki wa Simba wamehamasika, kila mmoja amehamasika kuhakikisha Simba inashinda na anaamini mchezo wa AS Vita utavuta mashabiki wengi.