Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Walichosema Wenger na Guardiola baada ya Carabao Cup (+picha)

3855 4996332C00000578 5433013 Image A 349 1519584306754 TZW

Sat, 3 Mar 2018 Chanzo: bongo5.com

Baada ya kikosi cha Manchester City kutwaa taji lake la kwanza kikiwa chini ya kocha wake raia wa Hispania, Pep Guardiola kwakuifunga Arsenal kwa jumla ya mabao 3 – 0 makocha wa pande zote mbili wamezungumzia mchezo huo.



Kwa upande wa Arsene Wenger  ameipongeza City kwa ubingwa huo huku akilaumu bao la pili kuwa lilikuwa ni la ‘offside’.

Pongezi kwa City kutwaa kombe, watarejea nyumbani wakiwa na furaha nasi tutarejea tukiwa tumepoteza.

Najiskia vibaya lakini najua tuna stahili kuadhibiwa kwakuwa tumepoteza nafasi na tumewapatia ushindi, goli la kwanza lilikuwa sahihi lakini lapili lilikuwa ‘offside’ kwa vile nilivyoona mimi.

City waliweza kuutawala mchezo na kufanikiwa kuibuka na ushindi nawapongeza kwa hilo.

Wakati unapopoteza mchezo kama huu kila mtu huoji kuhusu wachezaji, timu na mambo binafsi.

Lakini tumecheza na timu bora huwezi kusema walikuwa wakawaida.



Kwa upande wa meneja wa Man City Pep Guardiola amesema kuwa

Katika kipindi cha kwanza hatukuwa vizuri na tulifanya makosa mengi lakini kipindi cha pili tulirejea katika mchezo.

Lilikuwa muhimu kutwaa taji hili baada ya kutolewa katika michuano ya FA Cup na sasa tunaangazia taji la ligi tunahitaji kulitwaa na tunataka kuingia robo faibnali ya  Champions League.

Ushindi huu siyo wa kwangu bali ni kwa Manchester City wote

  
Chanzo: bongo5.com