Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wakimataifa wanogesha tizi la Taifa Stars

15626 Pic+stars TanzaniaWeb

Wed, 5 Sep 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Wachezaji Mbwana Samatta, Thomas Ulimwengu, Abdi Banda na Hassan Kessy wanaocheza soka la kulipwa nje ya nchi, wametua nchini na kujiunga na mazoezi ya Taifa Stars leo jioni kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Samatta anatokea Genk ya Ubelgiji, Ulimwengu (AL Hilal, Sudan), Banda (Baroka, Afrika Kusini) na Hassan Kessy (Nkana Fc, Zambia).

Nyota wanacheza soka la kulipwa na wanatarajiwa kuwasili muda wowote, Simon Msuva, Himid Mao, Farid Mussa na Shaban Chilunda.

Tanzania inajianda na mechi dhidi ya Uganda ya kusaka kufuzu kwa fainali za Mataifa ya Afrika mwakani nchini Cameroon.

Chanzo: mwananchi.co.tz