Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wakili Yanga Awapa Neno Bodi ya Ligi

Yanga 4?fit=613%2C383&ssl=1 Wakili Yanga Awapa Neno Bodi ya Ligi

Tue, 11 May 2021 Chanzo: globalpublishers.co.tz

Wakili Yanga Awapa Neno Bodi ya Ligi May 11, 2021 by Global Publishers



SAKATA la kuahirishwa kwa mechi ya Watani wa Jadi, Simba na Yanga, limezidi kushika kasi baada ya Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) kutoa taarifa ya kulipeleka suala hilo kwenye Kamati ya Masaa 72.

Ishu hiyo imemuibua mwanasheria wa zamani wa Yanga, wakili msomi, Frank Chacha ambaye ameitaka kamati hiyo kutenda haki kwenye shauri hilo.

Simba na Yanga walitarajiwa kupambana Jumamosi ya Mei 8, mwaka huu kwenye Dimba la Mkapa, Dar ukiwa ni mchezo wa Ligi Kuu Bara ambao awali ulipangwa kufanyika saa 11:00 jioni, kabla ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kutoa taarifa ya kusogezwa mbele hadi saa 1:00 usiku jambo ambalo Yanga hawakukubaliana nalo. Mechi ikaahirishwa.



Akizungumza na Spoti Xtra,wakili Frank amesema: “Kwa jinsi sakata hili lilivyo, si Simba wala Yanga ambao wanahusika moja kwa moja, Yanga walifuata kanuni na Simba walitii maagizo ya Shirikisho na Serikali, hivyo kila upande ulikuwa sawa kwa mujibu wa kanuni

“Nimesikia Bodi ya Ligi imelipeleka shauri hili kwenye Kamati ya Nidhamu, kwa upande wangu sioni mantiki yoyote ya sakata hili kupelekwa kwenye kamati hiyo kwani Simba na Yanga hakuna aliyevunja kanuni kwa mujibu wa kanuni za ligi zinavyoelekeza.

“Niwaombe TFF pamoja na Bodi ya Ligi sakata hili wasilichukulie juu au maamuzi yasitolewe juu juu kwani inaweza kuleta taharuki kubwa kwenye soka letu, hivyo natarajia kuona busara zaidi ikitumika kuliko kufanya maamuzi ambayo yataonekana kuupendelea upande fulani.

”Wakati sakata hilo likiendelea huku ikiangaliwa uwezekano wa mashabiki waliokata tiketi kurudishiwa fedha zao, kumekuwa na sintofahamu kama timu husika nazo zitarudishiwa gharama za kujiandaa na mchezo huo.

Mkurugenzi wa Mashindano ya TFF, Salum Madadi alipotafutwa na Spoti Xtra kubainisha hilo, alisema: “Katika hilo sijui chochote na siwezi kuzungumzia. Mtafute msemaji.”Alipotafutwa Ofisa Habari wa TFF, Clifford Ndimbo, alisema: “Nipo kwenye kikao kwa sasa.”

STORI: HUSSEIN MSOLEKA NA LUNYAMADZO MLYUKA

Chanzo: globalpublishers.co.tz