Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wajumbe TFF wang’aka

24f99843fd967460046570b93960c396 Wajumbe TFF wang’aka

Fri, 18 Jun 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

BAADHI ya wajumbe wa mkutano mkuu wa Shirikisho la soka Tanzania (TFF) wameshangazwa na wadau wa soka kuhoji suala la katiba na kanuni za uchaguzi wakati huu.

Wakizungumza na gazeti hili kwa nyakati tofauti jana, wajumbe hao ambao ni viongozi wa vyama vya soka vya mikoa na wa vyama shiriki walisema hakuna tatizo lolote kwenye katiba na kanuni na kwamba wanaohoji sasa hawana nia njema na soka lwa nchi.

Tangu kutangazwa kwa uchaguzi mkuu wa TFF uliopangwa kufanyika Agosti 7 mwaka huu, baadhi ya wadau wamekuwa akihoji kipengele cha elimu ya shahada kwa mgombea urais na udhamini wa vyama visivyopungua vitano kwa mgombea urais.

“Katika kwa mujibu wa taratibu hupitishwa na mkutano mkuu kisha inakwenda kwa msajili serikalini, katiba iliyopo ni halali na haina tatizo lolote kwenye suala la elimu,” alisema Blassy Kiondo Mwenyekito wa Chama cha Soka Rukwa.

“Halafu kwanini suala la elimu liibuke sasa wakati katiba ilibadilishwa jambo hilo tangu uchaguzi wa mwaka 2004 uliomuweka Tenga (Leodegar) madarakani, uchaguzi wa Malinzi (Jamal) kilikuwepo, hadi awamu ya kwanza ya Karia (Wallace) kilikuwepo nashangaa haya mambo yanaibuka leo kama walikuwa na hoja walitakiwa kuhoji mapema.”.

Kuhusu suala la udhamini kwa wagombea, Kiondo alisema lilishajulikana tangu utawala uliopita (wa Malinzi) ikiwa ni pamoja na kupunguza idadi ya wajumbe wa mkutano mkuu.

“Fifa walikuja wakazungumza na wadau mbalimbali na walikubali kanuni hizo ziwekwe, hao wanaopinga wanataka kuturudisha nyuma,” alisema Kiondo.

Mwenyekiti wa Chama cha Soka Dar es Salaam (DRFA), Lameck Nyambaya alisema wadau wengi wanachukua fomu za kugombea bila kusoma na kuelewa katiba na kanuni za uchaguzi matokeo yake wanaona kila kitu kipya wakati mabadiliko yalifanyika miaka mingi na kwa uwazi.

“Nashauri wadau wawe wanasoma katiba kabla ya kuchukua fomu,” alisema.

Mwenyekiti wa Chama cha Soka Mtwara, Athumani Kambi alisema katiba imepitishwa kwa kufuata taratibu.

“Suala la elimu lishafanyiwa uchaguzi mara tatu… lakini katiba si msahafu wakati wowote inabadilika tu lakini si sasa ambapo watuw anakwenda kwenye uchaguzi, watuache twende kwenye uchaguzi baada ya hapo watoe maoni yao na kama itaonekana yanahitajika basi yatafanyiwa kazi wasiturudishe nyuma,” alisema.

Saidi Sudi Mwenyekiti wa Tanga alisema yanayotokea ni matokeo ya watu kutotilia maanani mambo yanapofanyika.

“Jambo la elimu ni jema sababu mtu anajiongeza, mfano elimu ya kidato cha nne, hata serikalini inatumika sikuhizi, madereva na watu mbalimbali wameondolewa makazini kwa kukosa elimu ya kidato cha nne.”

Mwenyekiti wa Chama cha Soka Simiyu Osuri Kosuri alisema wadau wengi wanafuatilia matokeo kwenye mpira na kuzishangilia Simba na Yanga ndio maana mambo ya katiba waliyapa kisogo.

“Mfano suala la elimu lilianza tangu uongozi wa Tenga lakini kwa vile sasa hivi watu wana mambo yao wanatafuta sababu… suala la udhamini lipo duniani kote, hata uchaguzi mkuu wa nchi rais anazunguka mikoani kutafuta wadhamini kwa hiyo hilo sio jambo la kupigiwa kelele ni utaratibu tu,” alisema.

Mjumbe wa mkutano Mkuu wa TFF kutoka Kigoma Issa Bukuku alisema: “Mambo yote ni kwa mujibu wa katiba, elimu na suala la udhamini yalipitishwa muda mrefu sikuona yeyote akipinga… katiba huwa hairekebishwi kwa matakwa ya uongozi, inarekebishwa inapoonekana inafaa, kwa hiyo wadau watusubiri,” alisema.

Mwenyekiti wa Chama cha wachezaji, Sputanza, Mussa Kisoki alisema elimu inayopigiwa kelele imefanya wawe viongozi kwenye mpira.

“Mimi nashangaa wanataka wachezaji gani waongoze mpira, maana walio madarakani wengi wamecheza na kama suala kiongozi lazima acheze basi Kibadeni (Abdallah) angekuwa kiongozi mkubwa sana.” Alisema Kisoki.

Chanzo: www.habarileo.co.tz