Ikiwa zimesalia siku mbili kabla ya mtanange wa watani wa jadi, Afisa habari wa klabu ya Simba Haji Manara amesema kuwa amekuwa mgumu sana wakuzungumza na waandishi wa habari kwa kipindi hiki lakini baada ya kutwaa ubingwa ameahidi kusema sana hadi kufikia hatua ya kuwehuka.
Akizungumza na waandishi wa habari mapema hii leo Makao Makuu ya klabu hiyo, Manara amesema atasema sana baada ya kuchukua kikombe na kutoa ahadi kufikia hatua ya kuwehuka, lakini kwa sasa atasubiri kwanza na kuchomekea neno la Kihindi ‘deka jahega’ akisema kuwa maana yake ni kuweka hakiba.
Mimi ninazungumza vizuri sana nandiyomaana nipo hapa kwa mwaka wa nne sasa kukaa kwenye klabu kwa miaka hiyo siyo kitu cha mchzeo hizi klabu si unajua bwana kidogo nyanyu nyanyu, mzee mwaka wanne natimba tu na ukifanya mchezo mpaka 2040 Mungu akinapa uhai.
Nitumie nafasi hii kusema nimekuwa mgumu sana kuzungumza na waandishi wa habari kwa muda huu hasa kuelekea mchezo huu na hasa timu inapofanya vizuri kwasababu wakati mwingine mtu anaweza kukutega hivi na ukaingia alafu ukaonekana kama unaleta mbwembwe.Tutasema sana baada ya kuchukua kikombe nawaahidi, kama nitawehuka hivi lakini kwa sasa tusubiri kwanza Wahindi wanasema ‘deka jahega’ unaweka hakiba ndiyo tunachofanya kwa hivi sasa.
Tunatarajia washabiki wetu waje kwawingi sana wajaze uwanja kwasababu sisi ndiyo tunao jaza kwenye mechi yoyote inayotukutanisha sisi na wao au timu nyingine.