Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wagosi wa Kaya waizima Ruvu Shooting

Coastal Pic Data Wagosi wa Kaya waizima Ruvu Shooting

Sun, 18 Apr 2021 Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

Kocha Boniface Mkwasa amesema kipigo ilichopata timu yake ya Ruvu Shooting cha bao 2-1 dhidi ya Coastal Union kimetokana na kuzidiwa kimbinu.

Akizungumza katika uwanja wa Mkwakwani baada ya mechi baina ya Ruvu Shooting na Coastal Union kumalizika, Mkwasa alisema wachezaji wake pamoja na kuwazidi wa Coastal Union kwa stàmina lakini walizidiwa kimbinu.

"Mbinu na bahati zimeipa ushindi Coastal Union, tumekubali matokeo tunajipanga kwa mechi zijazo" alisema Mkwasa.

Naye Kocha wa Coastal Union, Juma Mgunda aliwapongeza wachezaji wake kwa kushinda mechi hiyo ambayo alisema ilikiwa ya muhimu kwake.

"Tuliingia kwa tahadhari kubwa kwa sababu ya aina ya wachezaji wa Ruvu Shooting na Mwalimu wao,Mkwasa mimi ni kiongozi wangu namheshimu na najua anajua kusoma mchezo na kubalisha" alisema Mgunda.

Ruvu Shooting ndiyo iliyokuwa ya kwanza kufunga bao lillilotiwa wavuni na Full Maganga dakika ya 20 lililotokana na krosi iliyochongwa na William Patrick.

Dakika ya 42,Coastal Union iliweza kusawazisha bao lililofungwa na Yussuf Chambo aliyeunganishiwa mpira wa juu uliotokana na kazi  nzuri iliyofanywa na Abushehe.

Bao la pili lililoipatia ushindi Coastal Union lilifungwa na Ayoub Masoud dakika ya 62 aliyepiga kona iliyoingia moja kwa moja kwenye nyavu za Ruvu Shooting.

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz