Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wadau walipowapa neno vijana wa U-17

51069 PIC+WADAU

Mon, 8 Apr 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Olipa Assah, Dar es Salaam

Wadau wa soka nchini, wametoa mitazamo yao kuelekea fainali za U-17 zaidi wakiwataka vijana wa Serengeti Boys kufahamu kuwa Watanzania wanasubiri kuona kombe linabaki Tanzania.

JAMHURI KIWHELO ‘JULIO’

Kocha wa zamani Dodoma FC, Jamhuri Kiwhelo ‘Julio’ ametaja mambo matatu ambayo wanapaswa kufanya Serengeti Boys ili kupata nafasi adimu ya kushiriki Kombe la Dunia la vijana wa umri wa chini ya miaka 17 ambayo ameyataja kuwa ni nidhamu, ufahamu juu ya kutegemewa na nchi pamoja na uzalendo.

DAN MRWANDA

Mchezaji wa zamani wa Simba, Yanga na Taifa Stars, Dan Mrwanda anasema kwa namna ambavyo amewaona Serengeti Boys, wana nafasi kubwa ya kufuzu kucheza Kombe la Dunia la vijana na anashauri Watanzania kuungana kwa pamoja kama walivyofanya kwa Taifa Stars.

SAIMON MSUVA

Supastaa Simon Msuva, anayecheza soka la kulipwa nchini Morocco, ameshauri kamati iliyokuwa imeundwa na mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kwa ajili ya Taifa Stars, waiendeleze mpaka kwa Serengeti Boys kuwasaidia kufika hatua ya kucheza Fainali za Kombe la Dunia la vijana chini ya miaka 17.

NURDIN BAKARI

Beki wa zamani wa Yanga, anasema ni zamu ya Tanzania kuandika rekodi ya kuvutia hata kucheza Fainali za Kombe la Dunia, akidai tayari Taifa Stars, imeonyesha njia kwa wadogo wao Serengeti Boys kwamba inawezekana na sio miujiza.

ALLY PAZI SAMATTA

Baba mzazi wa supastaa, Mbwana Samatta anasema Serengeti Boys ina nafasi kubwa ya kuishi ndoto za kucheza kutwaa ubingwa wa Afrika kwa vijana na kama wakikosa basi hata kukata tiketi ya Fainali za Kombe la Dunia la vijana. Anaamini watafanya vizuri kwa kuwa wameandaliwa vya kutosha, kilichobaki kuwaunga mkono.

ALLY MAYAY

Mchambuzi wa soka nchini, Ally Mayay Tembele anasema Serengeti Boys watambue uzito wa michuano hiyo na nafasi kuwa ya pekee, akitolea mfano wa Taifa Stars, iliyosubiri miaka 39 kufuzu AFCON na kwamba hata wao wasije wakafanya hivyo kwa kuwa Tanzania inawategemea“Kipaji bila utashi wa wachezaji ni kazi bure na hilo sio jambo la kocha wao, Oscar Mirambo, hivyo wakikutana na wavipaji kutoka nchi nyingine, utashi huamua matokeo, Watanzania nao kushangilia wasisubiri matokeo wanatakiwa kuanza dakika ya kwanza mpaka 90,”anasema.

ZAMOYONI MOGELLA

Staa wa zamani wa Simba, Zamoyoni Mogella amekiaminisha kikosi cha Serengeti Boys kwamba kina uwezo wa hali ya juu kupata ushindi katika mechi zake, wanachotakiwa ni kutuliza akili na kucheza mpira.



Chanzo: mwananchi.co.tz