Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wadau wafunguka kauli tata ya Karia

39915 Kalia+pict Wadau wafunguka kauli tata ya Karia

Mon, 4 Feb 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Muda mfupi baada ya Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Wallace Karia, kutoa kauli yenye utata kuhusu Mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), Tundu Lissu, wadau wa michezo wametoa maoni tofauti kuhusu matamshi ya kiongozi huyo.

Juzi katika Mkutano Mkuu wa TFF uliofanyika Arusha, Karia alisema hatasita kuchukua hatua kwa watu wenye tabia ya ‘uTundu Lissu’ katika soka na kamwe hawezi kukubali kuona wakiendelea kukosoa uongozi wa TFF.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti jana, wadau wa soka akiwemo Mwenyekiti wa zamani wa Baraza la Michezo Tanzania (BMT) Kanali Mstaafu, Idd Kipingu, alimtaka Karia kuomba radhi.

Kipingu alisema ni kosa masuala ya soka kupelekwa katika siasa kwa kuwa yanaweza kuchochea uvunjifu wa amani ndani ya nchi.

“Kama ameomba msamaha asamehewe, lakini anapaswa kutoa maelezo rasmi yakiwa yamerekodiwa kueleza hakuwa na maana hiyo ambayo watu wametafsiri na kuomba radhi pia, lakini awe makini sana na hayo matamshi,”alisema Kipingu.

Katibu Mkuu wa zamani wa TFF, Frederick Mwakalebela alisema anaamini Karia aliteleza kutoa kauli hiyo ndiyo maana baada ya mkutano alitambua kosa na kuomba radhi.

Alisema kauli ya Karia ina ukakasi kwa kuwa Chadema wakienda kushitaki Fifa pande zote mbili zinaweza kuitwa kutoa maelezo. “Wakipeleka Fifa pande zote mbili zinaweza kuitwa kutoa maelezo, kama unavyojua hawataki soka kuingizwa katika masuala ya siasa jambo hili siyo zuri,”alisema Mwakalebela.

Kocha wa zamani wa Taifa Stars Dk Mshindo Msola alisema kauli ya Karia haikuwa nzuri kwa kuwa soka na siasa ni vitu ambavyo havichangamani.

“Lazima ajue kwenye mpira kuna watu wa vyama tofauti na Fifa haitaki masuala ya mpira kuchanganya na siasa. Nafikiri ndio maana akatambua kuwa alikosea na kafafanua alimaanisha nini na akaomba msamaha, hivyo wamsamehe,” alisema Msola.

Mchambuzi Ally Mayay alisema suala hilo halipaswi kuendelea kukujadiliwa kwa ustawi wa soka na ametaka mjadala ufungwe ili kurejesha amani Chadema.

Baada ya kauli ya Karia, Chadema kupitia Mkurugenzi wa Itifaki, Mawasiliano na Mambo ya Nje, John Mrema alisema wamepokea kauli ya Karia kwa ukakasi kwa madai ilikuwa na lengo mahususi la kuwashughulikia watu wa aina ya Tundu Lissu



Chanzo: mwananchi.co.tz